Na Hafidhi Hamisi
NAIKUMBUKA sana bendi yetu ya shule kipindi nikisoma kama wewe sasa, enzi hizo nilikuwa nikipuliza filimbi kwa ustadi wa hali ya juu huku wanafunzi wakiimba wimbo wa Taifa.
Kila mmoja wetu aliimba kwa furaha, lakini siku hizi nafahamu wengi wenu hamjui hata beti chache za wimbo huo muhimu kwa Taifa.
Natambua wanafunzi wote mnasoma somo la Historia lenye mambo mengi mazuri ikiwemo historia ya nchi yetu. Lakini leo naomba tena kuwakumbusha historia ya nchi yetu.
Wanafunzi wengi wanachanganya kuhusu Tanzania na Tanganyika. Pengine hata wewe haufahamu kuwa kuna tofauti kati ya Tanzania na Tanganyika.
Wapo pia baadhi yenu wanaosema eti Tanzania ilipata uhuru. Hilo si kweli! Tanganyika ndio iliyopata uhuru tarehe 9, Disemba mwaka 1961 kupitia chama cha Tanu chini ya uongozi wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Baada ya hapo Tanganyika na Zanzibar zikaungana chini ya uongozi wa Mwalimu Nyerere na Sheikh Abeid Aman Karume wa Zanzibar na kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 26, aprili 1964.
Hapo ndipo neno Tanzania likaanza kutamkwa katika midomo ya watu na mpaka sasa tunajulikana kuwa ni Watanzania.
Lakini waasisi hao wa muungano wetu wameshatangulia mbele ya haki. Kwa mfano, mwalimu Nyerere alikufa Oktoba 14 mwaka 1999.Watanzania wengi tulipatwa na majonzi baada ya aliyekuwa Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa kutangaza kifo chake kilichotokea nchini Uingereza.
Marehemu Nyerere na waliokuwa viongozi wenzake enzi za uongozi wake, kwa pamoja walichukia rushwa na kuwakamata wale wote waliojihusisha na vitendo hivyo.
Pia kumbukeni kuwa tarehe 9, Disemba mwaka huu tutakuwa tukisherekea miaka 50 ya uhuru wetu kutoka kwa mkoloni Mwingereza.
Kwa sasa tukielekea katika siku hiyo, maonyesho na maadhimisho mbalimbali yanaendelea kufanyika huku lengo kuu likiwa kuonyesha mafanikio tuliyopata tangu uhuru. Je , wewe mwanafunzi unatambua mafanikio yapi ambayo umeyaona tangu uhuru mpaka leo?

No comments:
Post a Comment