Sunday, November 20, 2011

SERIKALI HAIONI AIBU KWA HILI LA POSHO ZA KUFUNDISHIA ZA WALIMU


Na Mdau Mwl JOHN K M.
0714229939.
 
      Itakumbukwa miaka ya nyuma serikali ilikuwa ikiwalipa walimu nchini posho zao za kufundishia.posho hii ilisaidia kumpunguzia makali ya maisha mwalimu sambambamba na kumuongezea ari ya kufanya kazi na moyo wa kujituma katika kazi kitu ambacho kilisababisha walimu kuheshimika sana katika jamii. Lakini kutokana na sababu zilizo nje ya ue...lewa wa walimu wengi naweza pia kusema karibu woote posho hii ilifutwa au kuondolewa. Walimu wamekuwa wakiipigia kelele serikali kila siku ili kurejesha posho hii na ikiwezekana iongeze na posho zingine kama vile “housing allowance”lakini serikali imekuwa ikipoga danadana tena cha kustaajabu hata baadhi ya viongozi ambao walimu walitegemea kuwatetea kwa kuwa na wao walipitia katika taaluma hiyo na hivyo wanajua shughuli ya ufundishaji wao wamekuwa kimya na huenda wakawa ndio wabaya zaidi katika kuwatetea walimu hata baadhi ya majibu wanayoyatoa katika vyombo kama Bunge hukatisha tamaa.
Mfano katika kujibu swali hili lililoulizwa na mh Pudenciana kikwembe lililouliza “Serikali imejielekeza kuboresha zaidi huduma za kijamii kama Elimu kwa kuajiri walimu wengi zaidi na kuchukua hatua ya kuboresha maslahi na mazingira ya kufanyia kazi ya walimu:-

(a)Je, Serikali haioni kuwa sasa ni wakati muafaka wa kurudisha posho ya kufundishia na posho ya nyumba kwa Walimu ili kujikimu na mazingira magumu ya kazi yao?

(b)Je, ni lini mpango kabambe wa kujenga nyumba za walimu kote nchi utaanza?

Sehemu ya majibu ya maswali hayo ilikuwa ….. “Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Pudenciana Kikwembe, Mbunge wa Viti Maalum, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

(a) ……..”Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua ukubwa wa kazi ya Mwalimu pamoja na mchango mkubwa anaoutoa kwa jamii pamoja na changamoto zinazomzunguka katika kutoa elimu nchini. Kwa kutambua ukweli huu, Serikali imeendelea kuboresha maslahi, mishahara na stahili za Walimu ili kuwapa ari ya kufanya kazi.

Katika maboresho hayo posho ya kufundishia na ya nyumba zilijumuishwa katika mishahara yao ili wanufaike, kwani inakuwa sehemu ya mafao yao wanapostaafu.

Kwa majibu kama haya inawezekana serikali ilitumia njia ingine tu mbadala ya kusema sasa serikali haiwalipi posho hizi walimu kwani matendo yao hujidhihirisha kabisa katika matendo.
Serikali inayochukulia kila kitu siasa mwisho wake hata inapoonesha dalili za kushindwa majukumu yake huchukulia kama mwenendo wa kisiasa, mwisho wake huanguka kwa kutokuwa na siasa makini.
Kama posho za kufundishia walimu zilijumuishwa kwenye mishahara yao mfano katika hali ya sasa kama mwalimu wa shahada mwenye basic salary ya 469000 aamue kutoa teaching allowance kama alivyojibu mh mshahara wake ‘basic salary’ itakuwa shilingi ngapi? ikiwa posho ilikuwa ni 50% ya mshahara.

Kama mwalimu wa shahada analipwa 469000
Na kwamba posho yake imejuishwa yaani aprox 50%
Na pia mshahara wake hatuujui tuuite X.
469000 =50%X + X

(469000)×2 = (50%X + X) ×2

469000×2= 3X

938000/3 = 3X/3

X = 312666

X = 312666 Ni mshahara wa mwalimu wa shahada kabla ya makato yeyote.

Is it fair? An insult like this?
Hivi huu ndio mshahara ‘basic salary’ ya mwalimu aliyehitimu digrii kutoka chuo kikuu? Akikatwa abaki na ngapi?
Sasa huyu ndiye wa digrii hawa wanaoanza na cheti watakuwa na pesa ngapi?

Mimi nafikiri viongozi wanaposimama kujibu hoja hii wasitubabaishe waseme wazi POSHO ZA WALIMU ZILIFUTWA. Kwani kuendelea na hoja ya kuwa zilijumuishwa kwenye mishahara yao wakati walimu wenyewe hawataki na ndio maana wanaidai kila siku ni kuendelea kudhalilishana.
Hata mh rais alishawahi kuagiza ufuatiliaji wa kero hii lakini kwa kuwa ni sekta ambayo inawagusa watu waliojichokea na kukata tamaa mpaka leo hakuna lolote linaloendelea.
Ninaamini uvumilivu wa walimu ndio sababu haki zao zimeendelea kupotea, na isiwe silaha kwa serikali kuendelea kuwakandamiza.
Imefikia hatua walimu hawana imani na serikali wala chama chao na ndio maana matokeo ya kazi zao katika mashule yameendelea kudorola kadili siku zinavyokwenda mbele. Hatima yake watoto wa masikini walio wengi wanapoteza muda mashuleni bila kuendelea kitaaluma hivi serikali haioni kuwa inaandaa bomu kubwa sana?
Mbona posho za idara zingine kama majeshi hazijumuishwi? Au leo zikijumuishwa mishahara yao itaongezeka au kubaki hivyohivyo kama ya walimu ilivyo? Huu ni wizi mtupu kwa walimu wetu. Tunatambua mchango na heshima waliyokuwa nayo walimu ambayo sasa imepotea.

Wakati umefika POSHO ZA WALIMU ZIRUDISHE na sio kutoa majibu yasiyojitosheza wabunge msiridhike na majibu hayo kama watu msiojua MAGAZIJUTO, Walimu lazima wawajengee uwezo vijana wetu mashuleni ili kuepuka kuchagua viongozi wasioweza kuwaletea maendeleo. Nawashauri walimu kujitokeza kudai haki zao kamwe wasinyamaze kusubiri kusemewa na mtu yeyote.
‘KATIKA MIAKA 50 YA UHURU WALIMU TANZANIA WALIINUKA NA SASA WANAANGUKA’.

3 comments:

Anonymous said...

NI TAARIFA NZURI SANA UNAJUA WALIMU WENGI HATULIONI HILI
HAWA JAMAA SERIKALINI HAWAWEZ KUONA UMUHIMU WA WALIMU KWA KUWA WATOTO WAO WANASOMA ULAYA,NO MATTER WHAT HII NI DANGANYA TOTO. WALIMU TUJITOKEZE JAMANI KUDAI HAKI ZETU TENA KWA VITENDO SIO KUNUNG'UNIKA TU MASHULENI.

Wakuwapa.brogsport.com said...

Sure huyu jamaa yupo sahihi eti kila siku utaskia "BIG RESULT" mbona hatuoni au kisikia "BIG SALARY " kwa walimu huu ni ugandamizaji wa walimu hebu tuamke jamani walimu

kassanda said...

walimu lazima tuwe na subira na magufuli maana huyu jamaa amekuwa yupo sahihi kabisa kwa maslahi yetu, tukiwa waalimu jamii inatuamini tuna uwezo wa kuona mbali pia na kusoma alama za nyakati hasa kwa walimu wa kike wao wanaelewa matayarisho ya kupika wali wa nazi ni tyofauti na matayarisho ya kupika pilau huyu mheshimiwahawezi kusimamia njia zote kwa wakati mmoja kwanza anatayarisha kinapokuwa tayari kwa maana ya udhibiti wa fedha za serikali ndipo watakapogeukia upande wa pili na angefanya haraka kuingia upande wa pili hatuoni kama wangenufaika watu wachache walioweka wafanyakazi hewa tukumbuke ni kama wiki moja na nusu zilizopita alikwishatoa zaidi ya shilibngi bilioni moja na nusu ikiwa ni mwanzo wa kuondoa kwanza malimbikizo ya madeni swala la kujadili sisi walimu liwe baada ya bajeti.
sasa hivi ni mapema mno