Thursday, December 1, 2011

MATATIZO YA TANGA KIELIMU MSIYAFUMBIE MACHO

Na mwalimu Mbaraka Awadhi, Tanga
   Halmashauri ya wilaya ya Korogwe walimu wa Sekondari wananyanyasika sana,ufikapo muda wa kwenda masomoni husumbuliwa mno kupewa barua za ruhusa na wakati mwengine hukataliwa kabisa hata kama wametimiza muda wa kufanya kazi unaotakiwa.

Kuna baadhi ya walimu ninao wafahamu waliandika barua za kuomba ruhusa tokea mwaka 2007 mpaka kesho hawajapata barua hizo, watendaji wamekaa kimya wengine mpaka wamemaliza masomo na kurudi kazini halmashauri haina habari.

Kibaya zaidi baadae wanakuja kutishia kuwafungia mishahara walimu wote walio masomoni bila ruhusa,sasa waungwana tufikiri, kama halmashauri imekaa kimya kiasi hiki bila ya kujibu barua za walimu kama waende masomoni ama la hawa walimu wafanfe nini?.

Nakushauri Waziri Mkuu sijui kama nawe utakua kama wenzio wengi wa CCM, Jaribu kuwabana wakurugenzi wako wachape kazi, pia wawe watenda haki kwa walimu na idara ya elimu kwa ujumla kwani zinanuka uovu, uonevu,dharau,u nyonyaji,ukanda mizaji,rushwa za ngono.

Tuache siasa iitwe siasa na Elimu iwe Elimu.

No comments: