Tuesday, November 29, 2011

UNAYAJUA MAJUKUMU YA AFISA ELIMU KWENYE SEHEMU YAKO? WANATEKELEZA HAYA? TUPIA JICHO HAPA

MAJUKUMU YA AFISAELIMU WA MKOA
  • Kuwakilisha Wizara ya Elimu na Utamaduni katika ngazi zote za kielimu katika Mkoa.
  • Kufafanua na kusimamia utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo, katika Elimu ya Awali na Msingi, Sekondari, Mafunzo ya ualimu, Elimu ya Watu Wazima na Vituo vya ufundi Stadi.
  • Kuwa Mshauri Mkuu wa Katibu Tawala wa Mkoa kuhusu mambo ya Elimu.
  • Kushughulikia upanuzi wa elimu ngazi ya Elimu ya Awali, Elimu ya Msingi, Elimu ya Ufundi, Elimu ya Watu Wazima, Elimu ya Sekondari na Elimu ya Ualimu.
  • Kusimamia maslahi ya walimu.
  • Kuratibu, kusimamia, kuendesha na kutathmini Mitihani ya Darasa la Nne na la Saba, Kidato cha Nne na cha Sita, Mafunzo ya Ualimu pamoja na Mitihani ya Ufundi katika Mkoa wake ukishirikiana na Baraza la Mitihani Tanzania na Wizara ya Elimu na Utamaduni.
  • Kufuatilia utekelezaji wa taarifa za Ukaguzi wa Shule na Vyuo.
  • Kusimamia utekelezaji wa kazi za Maafisaelimu wa Wilaya, waliopo katika Mkoa wake.
  • Kuratibu na kuchambua Takwimu za Elimu katika Mkoa kwa ajili ya mipango ya Maendeleo katika Ngazi za Wilaya, Mkoa na Taifa.
  • Kusimamia na kuendesha uchaguzi wa wanafunzi watakaojiunga na kidato cha kwanza katika Mkoa wake.
  • Kuratibu na kusimamia uhamisho wa wanafunzi wa Elimu ya Msingi na Sekondari ndani na nje ya Mkoa.
  • Kuruhusu kukariri kwa wanafunzi shule za msingi hadi darasa la 6 kulingana na taratibu zilizopo.
  • Kuwa mjumbe wa Bodi za Tume ya Utumishi kwa Walimu katika Mkoa.
  • Kuwa Mjumbe wa Bodi ya Wilaya, Vyuo vya Ualimu na shule za Sekondari katika Mkoa wake.
  • Kuwa Mwakilishi wa Afisa Elimu Kiongozi wa Elimu katika Mikutano ya Bodi inayohusu uendeshaji, mipango ya maendeleo, nidhamu, mapato na matumizi ya fedha za shule za sekondari na vyuo vya ualimu katika Mkoa wake kulingana na kifungu cha 10 cha sera ya Elimu na Mafunzo [1995].
  • Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na Katibu Tawala wa Mkoa.
MAJUKUMU YA AFISAELIMU TAALUMA WA MKOA
Kuwa na Msaidizi rasmi wa Afisaelimu wa Mkoa kuhusu:
  • Kufuatilia na kusimamia utekelezaji wa taarifa za Ukaguzi
  • Kubuni mipango ya mitihani na kusimamia utekelezaji wake
  • Kuhakikisha kuwa walimu wanaandikiwa taarifa za siri
  • Kukusanya, kuchanganua, kutuma na kutoa takwimu sahihi
  • Kubuni mipango ya kuendeleza na kuimarisha taaluma ya walimu na wanafunzi
  • Kuratibu shughuli za Jumuiya ya Vijana na Chipukizi
  • Kuandaa mahitaji na ugawaji wa walimu
  • Kuratibu huduma kwa wanafunzi
  • Kuratibu Mafunzo ya Walimu waliomo Kazini
  • Kufanya kazi nyingine atakazopewa na Afisaelimu wa Mkoa.
MAJUKUMU YA AFISAELIMU WA WILAYA
  • Kuwakilisha Wizara ya Elimu na Utamaduni katika ngazi zote
  • Kufafanua na kusimamia utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo, Sheria na Kanuni katika Elimu ya Watu Wazima na Ufundi Stadi.
  • Kutoa ushauri wa kitalaamu kwa Halmashauri ya Wilaya, Mji au Manispaa kuhusu masuala yote ya kielimu.
  • Kudhibiti matumizi ya fedha za elimu kwa mujibu wa miongozo ya fedha za Serikali.
  • Kushughulikia upanuzi wa Elimu katika ngazi ya Elimu ya Awali, Elimu ya Msingi, Elimu ya Sekondari, Mafunzo ya Ualimu, Elimu ya Watu Wazima na Vituo vya Ufundi Stadi.
  • Kufuatilia kwa madhumuni ya kutathmini maendeleo ya Elimu katika Wilaya.
  • Kutayarisha na kusimamia utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya Elimu kila mwaka.
  • Kuhakikisha kwamba shule zote zinaboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia.
  • Kuhimiza udhibiti wa nidhamu ya walimu na wanafunzi wilayani.
  • Kusimamia maslahi ya walimu.
  • Kuratibu na kusimamia mitihani ya Darasa la Nne, Darasa la Saba , Kidato cha Nne, Kidato cha Sita, Mafunzo ya Ualimu na Mitihani ya Vituo vya Ufundi Stadi katika wilaya kwa kushirikiana na Uongozi wa Elimu Mkoa na Baraza la Mitihani la Tanzania .
  • Kufuatilia Utekelezaji wa taarifa za Ukaguzi wa Shule na Vyuo.
  • Kusimamia Maendeleo ya Taaluma katika wilaya.
  • Kukusanya, kuratibu na kuchambua takwimu za elimu katika Wilaya kwa ajili ya Mipango ya Maendeleo katika ngazi ya Shule, Wilaya, Mkoa na Taifa.
  • Ni Katibu wa Kamati ya elimu na Utamaduni ya Halmashauri ya Wilaya/Mji/Manispaa kufuatana na kifungu cha 2 cha Sheria ya Elimu Na. 25 ya mwaka 1978 na kurekebishwa mwaka 1995.
  • Kufanya kazi nyingine kama utakavyoelekezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya.
MAJUKUMU YA AFISA ELIMU TAALUMA WILAYA
  • Kufundisha kila inapolazimika kufanya hivyo kwa lengo la kuonyesha mfano wa ufundishaji bora kwa walimu pamoja na kudumisha Ualimu wake.
  • Kufuatilia na kuhimiza uanzishaji na matumizi bora ya vituo vya walimu [Teachers’s Centers].
  • Kushirikiana na Wilaya katika kupanga na kuendesha semina, warsha na mikutano ya elimu ya ualimu.
  • Kuandaa mipango ya mafunzo ya walimu kazini na kushiriki katika kuwafundisha.
  • Kuhimiza na kushiriki katika kuendesha mashindano ya taaluma kwa wanafunzi wa shule za msingi.
  • Kushiriki kikamilifu katika kupanga na kusimamia mitihani ya madarasa ya IV na VII.
  • Kusoma taarifa za ukaguzi wa shule na kufuatilia utekelezaji wa ushauri unaotolewa na wakaguzi wa shule.
  • Kufanya tathmini ya mitihani ya darasa la IV na VII.
  • Kufanya utafiti wa mambo mbalimbali ya elimu wilayani mwake.
  • Kubuni mambo yanayoweza kuendeleza taaluma katika wilaya yake.
  • Kufanya ziara shuleni kwa lengo la kutaka kuzungumza na walimu kuhusu mafanikio na matatizo ya ufundishaji wa masomo.
  • Kufanya kazi nyingine za kielimu na atakazopewa na Afisaelimu wa Wilaya.

No comments: