Katibu mkuu wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi Bwana Hamis Dihenga amesema serikali ina mpango madhubuti kwa sasa kuteua baadhi ya vyuo kuanzisha chuo kitakachokuwa kikitumiwa na walimu watakaotaka kujiunga na masomo ya kujua namna ya kufundisha watoto wadogo (chekechea).
Aliyasema hayo jana katika mahafali ya kumi na mbili ya chekechea na mahafali ya pili ya kidato cha nne ya shule ya kiislamu ya Daarul Arqaam iliyopo morogoro.
Awali akifungua mahafali hayo mwenyekiti wa ISLAMIC FOUNDATION Bwana Arif Nahdi alisema kuwa kwa hakika anaishukuru kamati nzima kwa kuweza si kufanikisha tu bali waliojitolea pia michango yao mmoja mmoja mpaka shule hiyo kukamilika na kuwa miongoni mwa shule zinazoshika nafasi ya kwanza kwa miaka miwili mfululizo kwa upande wa primari na sekondari.
kwa kutilia mkazo Mh Dihenga alisema kuwa amefurhi kupatikana kwa eneo hilo na kwa waliojitahidi kupata eneo hilo mungu awazidishie na kwa kumalizia aliwasihi wazazi kuwa urithi mkubwa wa watoto ni elimu peke yake na kuwasihi wazazi kuwapeleka watoto wao shuleni kwani ndio kitu pekee kitakachowaokoa katika maisha yao watoto hao na kwa kumalizia alisema kuwa kwa wanafunzi wanaohitimu ndio kwaaanza wameianza shule hivyo kama safari ndio wanatakiwa wajifunge mkanda hapo na waongeze spidi ya kusonga mbele kielimu.

No comments:
Post a Comment