Monday, December 12, 2011

WANAFUNZI MANYONI WAJISAIDIA VICHAKANI



SHULE za sekondari za Chikuyu, wilayani Manyoni na Nduguti, wilayani Iramba mkoani Singida hazina vyoo hali inayowalazimu wanafaunzi kujisaidia kwenye vichaka.
Mratibu wa mradi wa Mfuko wa Uadilifu, Uwajibikaji na Uwazi, Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Uadilifu, Bernard Maendeleo Makoye, alisema hayo alipokuwa akitoa taarifa za changamoto walizokutana nazo wakati wakifanya tafiti kwenye shule za sekondari 14 zilizopo mkoani hapa kwenye semina ya kutatua changamoto katika usimamizi wa rasilimali za umma.
Alisema pamoja na changamoto hizo, utafiti huo ulibaini kuwepo kwa matumizi mabovu ya rasilimali katika shule ya Wembere, iliyopo katika Wilaya ya Singida Vijijini na Mitundu, iliyopo wilayani Manyoni.
Alisema licha ya shule hizo kuwa na majengo mazuri, lakini yameachwa kuwa nyumba za popo kwa kukosa wanafunzi na walimu.

No comments: