Makamu wa rais wa serikali ya wanachuo ya eckenforde akisisitiza jambo mbele ya waandishi, na pembeni ni baadhi ya wanachuo hao
Chuo cha eckenforde kilichopo Tanga Kimetakiwa kujisafisha la sivyo inabidi serikali iingilie kati kuchunguza juu ya namna chuo hicho kinavyoendeshwa kuanzia uongozi wa juu mpaka wahadhiri wake kuona uhalali wa chuo hicho ulivyo.
hayo yalisemwa na wanachuo wa chuo hicho walipozungumza na waandishi wa habari mbalimbali jana '' chuo hiki kinaendeshwa kienyeji sana angalia chuo kimeanza tangu mwaka jana february lakini mpaka leo hakina hata prospectus hiyo ni sawa?'' '' chuo kinaongozwa na sheria ndogondogo tu haiwezekani'' walisema wanachuo hao.
blog hii inaomba kutumia nafasi hii kukiomba chuo hicho kufanya haraka sana kuhakikisha kinajiendesha kisheria la sivyo tunaweza kukosa wasomi wenye tija katika taifa hili. na hii si tu kwa chuo cha eckenfode hata vyuo vingine ambavyo vina sifa hasi kama chuo hiki kikubwa.
No comments:
Post a Comment