Spika wa bunge la Tanzania Anna Makinda
Kujitetea juu ya kupanda kwa posho za wabunge kulikowasilishwa na mheshimiwa spika wa bunge Anna Makinda kumeonekana kama njama za makusudi za kujiongezea kipato pasipo maana kwani hoja ya kupanda kwa maisha huko Dodom HAINA MAANA YOYOTE KUSABABISHA WABUNGE HAO KUONGEZEWA MSHAHARA kwani hata huko Dodoma wapo walimu ambao mpaka leo wanaidai serikali na bado wanaishi maisha hayohayo ambayo leo serikali imeona yamepanda kwa mbunge
Pamoja na walimu ambao wanadai lakini pia bado walimu wanaendelea kupata pesa kidogo kama ujira wao kutokana na huduma ambayo wanaitoa kwa wanafunzi kama walimu, sitaki kusema vibaya lakini hili ni miongoni mwa mambo ambayo ukiangalia sana kwa makini utaona halikubaliki katika jamii hii ya kinyonge ya walimu watanzania ambayo inaendelea kuvumilia mambo haya huku ikiendelea kufanya kazi kwa bidii.
Kupitia mwnaharakati wa blog hii tunapenda kutoa maoni yetu kwa serikali kaa ikiendelea na lugha za kisiasa kuwa lazimisha watu kile wanachokiona ni sawa ipo siku walimu watachoka na kufanya maajabu makubwa kama kutofundisha kabisa kwa kukosa huduma muhimu makwao na hivyo kusababisha hasara kubwa kwa jaii ya watanzania hivyo serikali lazima iwe na busara za kutosha katika kuamua maamuzi kwani wajue jamii wanayoiongoza kwa sasa ni jamii ya wasomi na kila jambo linafuatiliwa kisomi hivyo ni lazima iwe makini.
No comments:
Post a Comment