WATOTO kadhaa huenda wakashindwa kuanza darasa la kwanza mwakani jijini Dar es Salaam kutokana na baadhi ya shule za msingi jijini humo, kuwatoza ada na michango ya kati ya Sh20,000 na Sh50,000 ili waandikishwe, Mwananchi imebaini. Uchunguzi wa gazeti hili uliofanyika kwa takriban wiki mbili, umebaini mbali na usumbufu huo wa michango na ada, kwenye baadhi ya shule, mtoto haandikishwi darasa la kwanza bila kuwa na cheti cha kuzaliwa au kadi ya kliniki.
Masharti hayo yameonekana kuwa mzigo kwa baadhi ya wazazi ambao wamekuwa wakilalamika na kuomba wapunguziwe michango hiyo bila mafanikio. Moja ya shule zinazotoza michango hiyo, ni Shule ya Msingi Nzasa iliyoko Temeke jijini Dar es Salaam ambako michango inatolewa kwa viwango vitatu tofauti, kuanzia Sh24,000, Sh36,000 na Sh40,000.

Mmoja wa wazazi waliofika shuleni hapo kuandikisha mtoto wake, Josephine Salehe aliliambia gazeti hili kuwa, "Niliambiwa na Mwalimu Mkuu nilipe Sh 40,000 ili mtoto aandikishwe." "Aliniambia (mwalimu mkuu) huu ni utaratibu wa kila shule. Kwamba ili kumwandikisha mtoto wazazi wanachangia. Wanahitaji kulipa Sh15,000, Sh6,000 kwa ajili ya fulana na Sh2000 kwa ajili ya kupigwa picha,"alieleza Josephine.
Josephine alitaja michango mingine aliyotakiwa kuchangia na viwango vyake kwenye mabano kuwa ni mlinzi (Sh2400), jengo (Sh10,000), nembo (Sh1,000) na fedha ya kuwalipa walimu kipindi wanapojitolea kuwafundisha wanafunzi ili kuyazoea mazingira ya shule (Sh1,500). “Mimi sina jinsi, hii shule kwangu nimeona ipo karibu na hatuna jinsi, inabidi nitoe Sh40,000 ili mwanangu aingie, nisipotoa mwanangu hawezi kuandikishwa hapa mwalimu mkuu anaangalia pesa tu,”alisema Josephine.
Mzazi mwingine Fredy Alphonce alisema aliambiwa na mkuu wa shule hiyo alipe Sh36,000 tu katika zoezi hilo la kumwandikisha mwanaye. Alisema baada ya kuambiwa atoe fedha hizo alijaribu kuzungumza na mwalimu na baadaye wakakubaliana alipe Sh24,000 tu. “Nilijaribu kubembeleza nipunguziwe na nikakubaliwa kulipa Sh24,000, lakini alinikatalia na kuniambia kama nimeshindwa wapo wenzangu wanazitafuta hizi nafasi,”alisema Alphonce ambaye alikuwa kwenye foleni ya kuingia kwa mkuu wa shule hiyo ili akalipe fedha hiyo.
Alipotakiwa kuzungumzia madai hayo, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Kahabi Mabeyo alisema wazazi wanapofika kuwaandikisha watoto wao, wanatakiwa kuwa vyeti vya kuzaliwa na fedha taslimu Sh26,400 ambayo ni mchango wa madawati (Sh15,000), nembo ya Shule (Sh1000) na fulana ya shule (Sh6,000). Alisema kuwa pia wanapaswa kulipa fedha ya mlinzi Sh2400 na fedha ya picha Sh2000. Hata hivyo Mabeho alikanusha madai kwamba mzazi asiyekuwa na fedha hiyo anazuiwa kumwandikisha mwanaye akisema kuwa sio kweli. "Kama hana leo, anamwandikisha mtoto wake ilimradi awe na cheti cha kuzaliwa na akipata fedha ataleta," alisema.
“Hii Sh1500 ya kuwalipa walimu ili kuwafundisha wanafunzi kabla shule hazijafunguliwa, hayo ni makubalino ya walimu na wazazi sio mchango wa shule," alieleza. Katika shule ya Msingi Kawe A, wazazi wanalazimika kutoa mchango wa Sh18,000 kwa ajili ya kuandikisha watoto wao wanaotarajia kuanza darasa la kwanza Januari mwakani. Mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo Moses Molel aliliambia Mwananchi jana kuwa kamati ilipitisha mchango wa Sh14,000 za kulipia huduma mbalimbali za shule hiyo pindi watakapoanza shule.
Alitaja aina ya michango kuwa ni Sh 5000 kwa ajili ya madawati, Sh 5000 ya ukarabati wa majengo ya Shule, Sh2000 ya mlinzi na Sh2000 kwa ajili ya bili ya maji. “Kikao cha wazi cha Novemba 19 kilikaa kujadili na kutoa mapendekezo ya kuwataka wazazi kulipia gharama za madawati, lakini pia kikao cha kamati kilipendekeza kila mzazi kulipia ukarabati wa majengo, gharama za mlinzi na bili ya maji,”alisema Molel. Molel alisema kiasi hicho cha fedha kinafanya jumla ya fedha wanazotakiwa kulipia wazazi kufikia Sh14000. Alifafanua kuwa shule hiyo inahitaji madawati 90 na kila dawati linagharimu Sh100,000 kwa mti wa Mninga na Sh90,000 kwa mti wa mpodo.
Alisema kutokana na hali hiyo, wazazi walikubali kulipa mchango wa madawati wa Sh5000 kila mmoja fedha ambazo zitakazosaidia kukamilisha kiwango kinachotakiwa kukusanywa kwa ajili y a kununua madawati hayo. “Mtaa huo una wazazi 936 na shule hiyo ya Msingi ina wanafunzi 1600 sasa, kati yao watoto 344 ni yatima wasioweza kulipia micnago hiyo”alisema Molel. Bila kufafanua kiasi kinachohitajika kuchangia kwa ajili ya madawati hayo, Molel alisema fedha hizo zitajazia pengo lililotokana na Sh1.2 Milioni zilizotolewa na manispaa hiyo kwa jili ya kununulia madawati.

No comments:
Post a Comment