Tuesday, December 13, 2011

MWANAFUNZI ATELEKEZWA NA WAZAZI WAKE HOTELINI

Mtoto Elly anaesoma shule ya msingi Bwawani darasa la sita iliyopo kiwalani wilaya ya ilala ametelekezwa na mama yake mzazi katika hoteli moja iliyopo mwanza ambae haikufahamika mara moja kuwa alikuwa na lengo gani

Mkurugenzi wa haki za binaadamu mama Kidjo Bisimba amesema suala lawazazi kuwatelekeza watoto wao ni moja ya matatizo makubwa na pia ni kosa kubwa na la jinai kwani ni sawa na kumharibia mtoto ndoto zake hivyo alisema ni bora suala hilo likachukuliwa kwa uzito wake.

Nae naibu waziri wa mambo ya jinsia na watoto Mh Ummy Mwalimu anasema hilo ni kosa kubwa sana, kwa kuiangalia sheria ya watoto namba 21 hivyo wazazi hao wanatakiwa kuchukuliwa hatua kali sana za kisheria, kwani mzazi wa kiume wa mtoto huyo ambae ni mkurugenzi katika sekta kubwa sana hapa Tanzania amekuwa akipiga chenga kuongea na waandishi wa habari licha ya kutafutwa kwa mara kadhaa na waandishi wa habari

Nae mkuu wa shule hiyo Bi Mayasa Mrisho amesema amesikitishwa sana na kupotea kwa mtoto huyo kwani ni takribani miezi tisa mtoto huyo hakuweza kuonekana shule na bila maelezo yoyote yale

Blog hii ina laani vikali suala hilo na kuomba serikali kuchukua hatua kali juu ya suala hilo

No comments: