Mwanamapinduzi ISLAM MPOSSO akiwa na NATALIE ambae ni afisa wa ICD katika moja ya warsha iliyoandaiwa na ICD usambara morogoro kwenye kuwawezesha walemavu haki zao nyingi ikiwamo ya kupata elimu sawa na wazima
Mwanamapinduzi ISLAM MPOSSO akishiriki kwenye moja ya miziki ambayo ilitungwa na yeye na kundi lake katika warsha ya kuwawezesha walemavu kielimu
Mwanamapinduzi ISLAM MPOSSO akiwafundisha wana warsha walemavu na wengine wengi namna ya kufanya harakati na jinsi ya kufuatilia haki zao za msingi juu ya kupata elimu bora na misingi ya ufuatiliaji wa uhalali wao kwenye harakati hizo.
Warsha iliyoandaliwa na ICD (Information centre on disability) Juu ya kuwajengea uwezo walemavu namna ambavyo watakavyopigania haki ya kusoma na dhana ya elimu jumuishi iliyodumu kwa muda wa siku tatu imemalizika rasmi wiki iliyopita huku wana warsha wakiwa wameshiba kwa yale waliyojifunza na wakiahidi kuyafanyia kazi katika maeneo yao walikotoka
ELIMU JUMUISHI NI MKOMBOZI WA WALEMAVU
No comments:
Post a Comment