Monday, December 12, 2011

MFUMO MPYA WA ADA HUUOOOOO!! WANUKIA!!


Naibu waziri wa elimu Mh. Philipo Mulugo

HABARI KWA HISANI YA GAZETI LA MWANANCHI

MFUMO  mpya wa kutoza ada kwa wanafunzi wa  shule zote nchini umekamilika na matumizi yake yanatarajiwa kutangazwa wakati wowote kuanzia sasa.
Akizungumza na Mwananchi  wiki iliyopita, Naibu  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,  Philipo Mulugo, alisema mchakato wa kukusanya maoni umeshakamilika  na kwamba kinachosubiriwa ni taratibu za mwisho.

Alisema ada za sasa zinalipwa kwa maelekeo ya  waraka namba 19 wa mwaka 2002 ambao ulipanga ada kwa wanafunzi wa shule za sekondari binafsi za bweni kuwa ni Sh 380,000 kwa mwaka na za kutwa Sh 150,000.
Halisema hata hivyo wamiliki wa shule hizo hawafuati kabisa maelekezo hayo.

 Naibu waziri alisema badala yake, wamiliki wa shule hizo wamekuwa wakijipangia ada bila kufuata maelekezo ya waraka huo.
Mligo alisema hali hiyo imeilazimisha Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, kuanzisha  rasimu ya maoni kutoka kwa wadau ili kuamua kwa pamoja, viwango vya ada kwa shule za Serikali na binafsi nchini.

Alisema tume iliyokuwa imepewa jukumu hio, imeshakamilisha kazi yake na kinachosubiriwa sasa ni kutangaza.
“Wizara yangu itahakikisha viwango vya ada vitakavyotangazwa vinazingitia gharama halisi ya kila mwanafunzi na kuweka uwiano katika ulipaji na utoaji ada,” alisema Mulugo.Elimu ni huduma si bidhaa kama zilivyo bidhaa nyingine, ambazo faida ni kichocheo kikubwa cha kuwekeza,” alisema.
Alisema jamii ya Tanzania inapaswa kupata elimu na kwa msingi huo wamiliki wa shule lazima wajali vipato vya Watanzania.

Kwa mujibu wa waziri huyo, utaratibu huo unategemewa kuanza kutumika mapema mwakani.
”Taasisi, mashirika na watu binafsi wanaotoa huduma za elimu wanapaswa kusaidia Serikali na si kuwakomoa wananchi,” alisisitiza.

No comments: