Monday, December 12, 2011

MKUU WA MKOA MWANTUMU MAHIZA AWASHANGAA WANAFUNZI SEKONDARI WASIOJUA KUSOMA WALA KUANDIKA


Mkuu wa mkoa wa pwani Mh. Mwantumu Mahiza

Habari na mwanamapinduzi kibaha,

Afisa elimu mkoani pwani Waliombora Nkya akiri kuwa kuna idadi ya wanafunzi wengi ambao wapo katika shule za sekondari mkoani humo hawajui kusoma wala kuandika.

Afisa elimu huyo alibainisha hayo mbele ya mkuu wa mkoa wa pwani Mh. Mwantumu Mahiza alipokuwa akizungumza na wakuu wa shule za sekondari mkoani humo na kusema kuwa hayo yametambuliwa kutokana na idara za elimu mkoani humo kufanya ukaguzi kwa baadhi ya shule mbalimbali nakutoa taarifa hiyo.

kwa upande wa Mh. Mahiza alisikitishwa na utaratibu wa kuchagua watoto hao kuingia katika shule hizo za sekondari kwani ni jambo la kushangaza. ''Inawezekanaje mtoto kuingia kidato cha kwanza ikiwa hajui kusoma wala kuandika?'' alisema mahiza.

Mh. Mahiza aliwaagiza wakuu wa shule hizo kufuatilia kwa undani sababu zilizofanya matatizo hayo kutokea kwani hatapenda tena mambo hayo yatokee tena katika mkoa wake na alimaliza kwa kuitaka idara ya elimu kuhakikisha mkoa huo unakuwa miongoni mwa mikoa inayofanya vizuri kielimu na kuongoza kabisa.

No comments: