ZAIDI ya Sh17 milioni zilipatikana katika harambee ya kusaka Sh30 milioni za ujenzi wa Sekondari ya Kipoka iliyopo kwenye Kata ya Makongorosi wilayani Chunya juzi.
Harambee hiyo iliandaliwa na Muungano wa Wachimbaji Madini mkoani Mbeya (Mberema)Tawi la Chunya, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Deodatus Kinawiro.
Akizungumza kabla ya michango kuanza, Mwenyekiti wa Mberema, Lusajo Ambakisye alisema waliamua kuanzisha harambee hiyo ili kusaidiana na Serikali katika kutekeleza miradi ya jamii hususani masuala ya elimu.
“Katika kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru, Mberema imeona ni busara kushirikiana na Serikali katika masuala ya maendeleo ya elimu wilayani Chunya”, alisema.
Alisema kwa kuanzia Mberema inatoa Sh3 milioni na kuwataka watu mbalimbali waliojumuika kwenye Ukumbi wa D.O uliopo Makongorosi kuanza kuchangia fedha na hata vifaa vya ujenzi.
Kufuatia kauli hiyo, Mkuu wa Wilaya Kinawiro alisimama na kuanza kuwahamasisha watu watoe fedha jambo ambalo waliitikia na kutoa fedha huku wengine wakiahidi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Maurice Sapanjo aliahidi kutoa mifuko 100 ya saruji.
Nayo Ofisi ya madini Wilaya ya Chunya iliahidi kutoa Sh 600,000.
Michango iliendelea na hatimaye hadi mwisho ilielezwa kwamba zaidi ya Sh17 milioni zilipatikana .
Akizungumza baada ya michango hiyo, mkuu wa wilaya aliwashukuru watu wote waliochangia na kuwataka watambue wazi kwamba suala la elimu ni muhimu kuliko michango ya harusi na mambo mengine ya starehe.
Shule ya sekondari Kipoka kwa sasa ina vyumba vitatu vya madarasa lakini linahitaji kukamilisha jengo la utawala na walimu ili shule hiyo iweze kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza mwakani.

No comments:
Post a Comment