WASICHANA wapatao 10 hivi wakionekana wachovu huku wamebeba mizigo vichwani walitembea taratibu kuelekea Shule ya Sekondari ya Rubanga iliyopo kata ya Kitahana wilayani Kibondo, Kigoma.
Baadhi yao walicheza ‘kidali po’ na wengine walitaniana mradi tu waliifanya kuwa fupi na ya furaha safari yao kiasi cha kilomita tatu hivi kutoka Kitahana walikoenda kusaga unga.
Mambo mawili ndiyo yaliwatambulisha wasichana wale kuwa ni wanafunzi. Kwanza ni uelekeo wao kwani njia waliyopita hakukuwa na majengo mengine isipokuwa ya shule, na pili walikuwa wamevaa sketi zinazofanana.
Baada ya dakika 20 hivi, nikiwa ndani ya ofisi ya Mkuu wa shule hiyo, Fulgence Misigaro, mwalimu wa zamu alikabiliana na wasichana wale.
“Kwa nini mmechelewa?” alifoka mwalimu yule na kila mmoja wao alipotaka kujibu mwalimu aliwatupia maswali mengine; “Mlikuwa wapi mpaka sasa? Mbona wenzenu walishafika mapema? Mmeanza mambo yenu eeh?”
Baadhi ya vyumba katika jengo la utawala ambavyo vilipaswa kuwa ofisi za walimu vimetengwa kama stoo ya chakula. Mahindi kwa ajili ya chakula na maharagwe kwa ajili ya mboga yaliyoletwa na wanafunzi wa hosteli yamewekwa humo.
“Hapa tuna hoteli kwa ajili ya wasichana yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 72 tu, lakini mpaka sasa wapo 56. Hawa wako chini yetu hivyo, lazima tuwadhibiti, walioko mitaani si rahisi kuwafuatilia,” anasema.
Uongozi wa shule hiyo umeweka utaratibu kwamba wazazi wa wanafunzi wachangie mahindi kwa ajili ya chakula cha mchana kiasi cha madebe matatu na maharagwe kiasi cha makopo 10.
Pamoja na utaratibu huo mzuri bado kuna baadhi ya familia zinashindwa. Familia nyingine ni maskini sana lakini nyingine hazijali umuhimu wa elimu kwa watoto wao.
“Wapo watoto wanaoacha shule kwa sababu ya kukosa chakula. Wanajiuliza watapata wapi hela za kununulia madaftari maana wengine hawana hata sare za shule; waliporuhusiwa waje na nguo za nyumbani bado imeshindikana,” anasema.
“Wanaoishi hosteli wanaendelea vizuri lakini wengine wanaona shida kula ugali kwa maharagwe kila siku na wakiugua hapa inabidi wajigharimie. Wanafunzi wawili wamepata mamba,” anasema.
Matatizo makubwa ya shule hiyo, kwa mujibu wa mkuu wa shule, ni uhaba wa walimu, kitabu kimoja wanafunzi 30, ukosefu wa maabara, ukumbi wa mikutano, bwalo, jiko na nyumba za walimu na mbaya zaidi shule haina Bodi, kwani iliyopo imevunjwa.
Ugumu wanaopata walimu wa Shule ya Sekomdari ya Rubanga kudhibiti nidhamu ya wanafunzi wanaoishi nyumba za kupanga ndio unawakabili walimu wa Shule ya Sekondari ya Kasange kata ya Karunga wilayani Kasulu.
Mkuu wa shule hiyo, Henry Mpabandi anasema kuwa wanapojaribu kuwafuatilia wanafunzi hao hasa wa kike, huambiwa na wazazi wao wanawanyima uhuru.
“Wanafunzi wetu wengine wanaishi katika mazingira magumu, inakuwa vigumu kudhibiti nyendo zao na mahudhurio,” anasema.
“Tunapowafuatilia tunaambiwa tunawanyima uhuru. Baada ya kupata changamoto hii tumeamua kufanya kazi kwa ushirikiano na wazazi, tunawaita waje shuleni ili tuzungumzie matatizo ya watoto wao,” anafafanua.
“Tuliwaita wazazi wanane ili tuzungumzie nao kuhusu waliko watoto wao. Wazazi hao wakasema watoto wao hawataki shule,” anaeleza Mpabandi.
Mbali ya baadhi ya wanafunzi kuacha shule na wazazi wao kutofanya juhudi kuwarejesha shuleni, mazingira walikopanga yanawakatisha tamaa ya kusoma, hivyo mara kwa mara hulazimika kwenda nyumbani katikati ya wiki.
Umaskini wa familia unachangia kwa kiasi kikubwa wanafunzi kuacha shule kwani baadhi ya wanafunzi hukosa fedha za kununulia madaftari, viatu na hata sare za shule.
Kasange, kama ilivyo kwa Rubanga inakabiliwa na matatizo ya miundombinu – nyumba za walimu, vyumba vya madarasa, maabara na hosteli kwa ajili ya wanafunzi.
Matatizo mengine makubwa katika shule hiyo ni uhaba wa walimu, ukosefu wa watumishi wasio walimu, ucheleweshaji wa ruzuku, na kudorora kwa makusanyo ya ada.
Tofauti na Rubanga na Kasange, kilio kikubwa kwa wakuu wa shule za sekondari za Malagarasi, Kibondo, Hwazi na Bogwe ni utoro wa wanafunzi kutokana na kupata mimba.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Malagalasi, Kibondo, David Mashauri anasema mwaka 2009 wasichana watatu walipata mimba na kuacha masomo, mwaka 2010 wasichana wawili walikatiza masomo kwa tatizo hilo na hadi Julai mwaka huu wasichana wanne wameacha masomo.
Katika Shule ya Sekondari ya Wasichana, Kibondo kati ya mwaka 2006 na 2010 zaidi ya wasichana 15 walipata mimba na kuacha shule. Baadhi wameolewa na wengine wako mitaani.
Mkuu wa shule hiyo, Ruth Msweti anasema robo tatu ya utoro wa wanfunzi katika shule hiyo ni mimba.
Ripoti ya Shule ya Sekondari ya Bogwe wilayani Kasulu iliyotolewa na Kaimu mkuu wa shule hiyo, Solomon Herson inaonesha kuwa wasichana saba wameacha masomo kati ya mwaka 2008 hadi sasa.
Chanzo
Mashauri anasema chanzo cha mimba mashuleni ni pamoja na malezi mabovu. “Ninachokiona hapa ni tabia ya kutegeana kati ya pande mbili – shukle na wazazi – katika kudhibiti watoto hivyo hupelekea uhuru mkubwa shuleni au nyumbani na matokeo yake ni kupata mamba,” anasema Mashauri.
Mkuu wa shule ya Hwazi iliyoko Kasulu, Richard Sabuni anasema kuwa licha ya kuwasihi wazazi mara kwa mara kuwasiliana na uongozi wa shule kuhusu maendeleo ya tabia ya watoto bado mwitikio ni mdogo.
“Sisi tunajitahidi tunapokuwa nao hapa kwa saa kama nane hivi, lakini baadaye wanapoondoka inatakiwa wazazi kuwajibika vilivyo pale nyumbani,” anasema Sabuni.
Naye Ruth anasema licha ya sheria kadhaa kuainishwa, pale inapobainika mtu fulani anahusika na ujauzito, sheria hiyo inakuwa haina tija.
“Hili ni tatizo na kwa mtindo huo hakuna mamlaka inayochukua sheria, si mtendaji wa kijiji au polisi. Hata uongozi wa shule ukifuatilia kushinikiza sheria ichukue mkondo wake kwa muhusika, hauungwi mkono kwa vile mzazi anakuwa amelamba kitu na viongozi wanatishiwa uhai,” anasema Ruth.
Moja ya matukio yaliyowakatisha tama ni askari mmoja wa Jeshi la Magereza mjini Kibondo ambaye alimpa ujauzito mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari Malagalasi mwaka 2009. Uongozi wa shule ulifuatilia lakini mambo yalimalizwa kinyemela na wazazi licha ya sheria kuwa wazi.
Mmoja wa wazazi katika shule hiyo, Joyce Habuga anasema kuwa umaskini na tamaa ya vitu kama simu za mkononi, na fedha za matumizi ya anasa. Mzazi huyo anapendekeza umaskini ukabiliwe ili kuondokana na vishawishi.

No comments:
Post a Comment