Thursday, November 10, 2011

WANAOUA SHULE YA SEKONDARI KISHOJU HAWA HAPA



Na mwandishi wetu muleba (MDAU)
Ni sisi wazazi na majirani wa Shule ya Sekondari Kishoju:
Rweyasiza G. Martin   0756 610 483
Twahiru Kawaya   0754 244 966
Hamidu Abdalah 0756 069 208 
Joseph Bisimbi 0768 227 235
SISI wazazi na wakazi wa Kata ya Magata Karutanga, Wilaya ya Muleba, tunasikitishwa na matukio yanayohusisha ofisi ya uongozi wa sekondari wilayani.
Afisa Elimu amejifanya “alpha na omega” katika elimu ya sekondari wilayani.
Katika siku za karibuni tumeshuhudia maendeleo kitaaluma ya kidato cha V na VI katika shule hii. Lakini shule imeshuhudia hivi karibuni vurugu za wanafunzi ambazo hazijengi.
Kwa mfano, usiku wa tarehe 9/05/2011, wanafunzi walivamia nyumba za walimu na kusababisha walimu na familia zao kukimbilia porini.
Mali za walimu na shule ziliharibiwa. Vurugu hizi zilitulizwa kwa msaada wa polisi.
Uongozi wa shule ulikaa na kubaini viongozi wa vurugu na kuomba bodi ya shule iwachukulie hatua wanafunzi wahusika.
Uamuzi ulifanywa lakini Afisa Elimu Sekondari wilayani alitaka maamuzi ya bodi yasitekelezwe bali yapelekwe kwake.
Mpaka tarehe tunapoandika haya, miezi mitatu na wiki mbili baada ya tukio, hakuna mwanafunzi aliyeadhibiwa kutokana na tukio hili. Huu ni udhalilishaji wa bodi ya shule na walimu.
Afisa Elimu Sekondari amekuwa na tabia ya kukutana na wanafunzi mara kwa mara shuleni na nje ya shule bila kuhusisha uongozi wa shule; na kila akikutana nao hatoi taarifa au maelezo kwa uongozi wa shule.
Kila baada ya mikutano hii wanafunzi wameonyesha kutowajali walimu na hasa wale wanaohusika na malezi na nidhamu.
Tuna wasiwasi vurugu za wanafunzi zilichochewa na vikao hivi vya afisa elimu na wanafunzi.
Hali hii imesababisha baadhi ya walimu kuondoka shuleni moja kwa moja kwa usalama wa maisha yao.
Walioondoka ni Mwalimu Shibitali anayefundisha Historia kidato cha V na VI. Wengine ni Mwalimu Colnel Kashaba (yuko Sekondari Buleza), Abubakari Kagambo na Juma Hamis. Walimu wengine wamo mbioni kujitafutia nafasi katika shule nyingine.
Kwa uthibitisho waweza kuwasiliana na walimu wenye simu hizi: 0783 046734, 0756 357782, 0756212848 na 0757826330.
Tangu tukio la walimu kuvamiwa usiku, walimu 12, (wanne wa kudumu na wanane wa mazoezi – BTP), wameondoka na hakuna mwalimu hata mmoja aliyeletwa kujaza nafasi zao. Sasa vipindi vingi havifundishwi.
Tunasikitishwa pia na uongozi wa elimu wilaya kumhamisha na kumteremsha cheo Mkuu wa Shule, Costa Paul (0756 357782), baada ya vurugu za wanafunzi.
Tumefanya kazi naye. Tunamjua na wanafunzi makini wanamthamini. Anakubalika hata kwa walimu wenzake kiwilaya.
Tunajiuliza je, vurugu za wanafunzi zilipangwa ili kupata njia ya kumwadhibu mwalimu huyu?
Tangu mwaka 2002 shule ilipokabidhiwa kwa uongozi wa wilaya yetu hatujawahi kupata kiongozi wa shule hii anayejali taaluma na nidhamu ya wanafunzi kama Paul.
Paul ametushirikisha kuinua taaluma na nidhamu. Ameboresha miundombinu. Mwaka jana aliongoza ujumbe wa shule kwenda Ujerumani na wafadhili wakaipa shule fedha kujengea maabara ya sayansi.
Sisi wazee tuliofanya kazi na Paul, tunajua ni hazina katika wizara ya elimu.
Tunashauri ufanyike uchunguzi juu ya kuondolewa kwake na kushushwa cheo. Kama ni kwa chuki binafsi, wahusika wawajibishwe na yeye asafishwe.
Kuna minong’ono kuwa Afisa Elimu Sekondari alitofautiana na mkuu wa shule katika suala lililohusu mzabuni. Hili nalo lichunguzwe.

No comments: