WANAZUONI nchini wameshauriwa kujenga tabia ya kusoma vitabu ili
kujenga utamaduni wa kuandika vitabu vitakavyosaidia kurithisha vizazi
taaluma walizonazo kwa faida ya jamii na taifa.
Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam jana na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa Joseph Kuzilwa, alipozindua kitabu cha Menejimenti ya Rasilimali Watu kilichoandikwa na mmoja ya wanazuoni wa chuo hicho, Profesa Josephat Itika.
Kitabu hicho kinapewa jina la ‘Fundamentals of Human Resources Management’ kitatumika kama rejea kwa wanafunzi wa elimu ya juu.
“Tunamshukuru msomi mwenzetu ameweza kuandika kitabu hiki pamoja na kwamba ana majukumu mengi, lakini ameweza. Hii inatoa fundisho kwetu sisi kama wanazuoni kuweza kuandika vitabu, ili wanafunzi waweze kuwa na vitabu vingi na vinavyoendana na mazingira ya Kitanzania,” alisema Profesa Kuzilwa.
Alisema kitabu hicho amekiangalia kwa undani na kinahusu Menejimenti ya Rasirimali Watu na kina visa vya Afrika na Tanzania kama inavyofahamika vitabu vingi vinavyotumika nchini vina hadhi ya Kimagharibi hivyo kitabu hicho ni muhimu kwa wanafunzi, watumishi wa umma na kampuni binafsi kupata ujuzi.
Alisema kitabu hicho kimeandikwa kwa msaada wa miradi inayofadhiliwa na Shirika la Serikali ya Uholanzi (NOFIC) ambalo limekuwa likisaidia miradi mbalimbali chuoni hapo.
Alisema Profesa Josephat Itika mbali na kuandika kitabu hicho pia ameteuliwa kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Taaluma na pia ni Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu, hivyo kazi aliyoifanya ni kubwa.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Utawala na Fedha, Profesa Faustin Kamzola, alisema wanazuoni lazima wajenge tabia ya kuandika vitabu ili kuchangia wanafunzi na wasomi walioko makazini kuweza kupata ujuzi zaidi unaoendana na Tanzania kwa ajili ya kuchochea maendeleo ya nchi.

No comments:
Post a Comment