
Mwalimu Cindy Clifton
Mwalimu wa kike wa nchini Marekani mwenye umri wa miaka 41, anakabiliwa na kifungo cha kwenda jela miaka 60 kwa kosa la kufanya mapenzi na wanafunzi wake wa kiume 11 katika kipindi cha miezi mitatu.
Mwalimu Cindy Clifton mwenye umri wa miaka 41 anakabiliwa na kifungo cha muda mrefu jela kwa kosa la kuwanywesha pombe wanafunzi wake wa 11 wa kiume wenye umri kati ya miaka 14 na 17 na kisha kufanya nao mapenzi.
Taarifa ya televisheni ya ABC ilisema kuwa mwalimu huyo wa shule ya msingi ya Crestview Middle School aliwalewesha wanafunzi wake wakati wa sherehe alizoziandaa kwenye nyumba yake na kufanya nao mapenzi katika kipindi cha kuanzia aprili 11 hadi julai 15.
Mwalimu huyo aliyejizolea umaarufu katika shule hiyo kutokana na ufundishaji wake anakabiliwa na mashtaka ya kufanya mapenzi na watoto wenye umri mdogo usiofika miaka 18.
Miongoni mwa wanafunzi waliofanya mapenzi na mwalimu huyo, walikuwa ni marafiki wa binti wa mwalimu huyo.
Mwalimu huyo alifunguliwa mashtaka miezi mitatu baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa polisi ulioanzishwa baada ya malalamiko mengi toka kwa wazazi.
"Uchunguzi wa polisi ulianza baada ya malalamiko ya wazazi ambao walilalamika watoto wao walinyeshwa pombe kwenye sherehe zilizoandaliwa na mwalimu Clifton", ilisema taarifa ya polisi.
Clifton amefunguliwa mashtaka 14 ya ubakaji na mashtaka 14 ya kuwanywesha pombe watoto.
Clifton ameachiwa kwa dhamana ya dola 40,000 na atapandishwa kizimbani tena Novemba 10. Huenda akahukumiwa miaka 60 jela iwapo atapatikana na hatia.
No comments:
Post a Comment