Wednesday, November 23, 2011

MAMBO HAYA YATAKWISHA LINI

 

Hapa sio bombani ni shuleni ambapo viti vimepangwa mahsusi kwaajili ya kusubiri wanafunzi wa kidato cha tatu kufanya mtihani, mpiga picha wa blog hii alikutana na kituko hiki kwenye moja ya shule ambayo inapatikana kati kabisa mjini morogoro sasa sisi kama wadau na wapenda elimu nchini tanzania tunajiuliza mambo haya yatakwisha lini?

hivi ni kweli kabisa kwa kijana ambae anafanya mtihani hapa ataweza kushindana na mwanafunzi ambae anafanya mtihani kwenye sehemu nzuuri kabisa kwenye shule za seminari? hii ni ngumu sana tunashauri serikali kuzifatilia shule hizi, kuna habari kuwa kuna baadhi ya sehemu serikali hutoa pesa kwaajili ya kuziendeleza shule hizi lakini baadhi ya wakuu wa shule wanatumia pesa hizo kwa manufaa yao.

No comments: