Thursday, November 17, 2011

WANAFUNZI 24 WAPATA MIMBA KENYA ABAKIA MMOJA TU DARASANI



NewsImages/2995150.jpg

Ni mwanafunzi mmoja tu wa kike katika shule moja ya sekondari nchini Kenya amebaki darasani baada ya wanafunzi wenzake wote 24 wasichana kuacha shule baada ya kupata mimba.
Mwanafunzi mmoja wa kike katika shule ya sekondari ya Marinyn Secondary School iliyopo katika mji wa Kericho nchini Kenya, amelazimika kujisomea mwenyewe baada ya wanafunzi wenzake wote 24 wa kike kuacha shule kwasababu ya ujauzito.

"Hali inasikitisha sana " alisema Samuel Njora mkuu wa wilaya ya Kericho..

"Hivi sasa wamebakia jumla ya wasichana 20 tu shule nzima na wasichana wengi wa madarasa ya juu wameacha shule baada ya kupewa mimba na wafanyakazi wa mashamba ya chai", alisema mkuu huyo.

Maafisa wa serikali wanalaumu umbali wanaotembea wanafunzi hao kwenda shuleni wakikatiza mashamba ya chai ya James Finlay kuwa ndio chanzo cha wasichana hao kupewa mimba na wafanyakazi wa mashamba hayo.

Njora alisema kuwa shule hiyo ya sekondari inabidi iwapatie usafiri wanafunzi wake wa kike kutoka majumbani mwao na kuwarudisha majumbani mwao ili kupunguza idadi ya wanafunzi wanaopata mimba.

Alisema kuwa wasichana wa form one wanakabiliwa na hatari ya kupata mimba kutokana na kuhadaiwa na wavulana na wafanyakazi katika mashamba ya chai wakati wa safari yao ya kuelekea shule.

Gazeti la The Standard la Kenya lilisema kuwa elimu kwa wasichana ni kama ndoto ya kutisha nchini humo.

Wasichana wengi hulaghaiwa na kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi yanayopelekea wapate mimba zisizotarajiwa.

Matokeo yake wasichana hao huacha shule na kuanza maisha ya kama wazazi.

No comments: