Thursday, November 17, 2011

TAFITI YAONYESHA WALIMU HUWAWEKEA WANAFUNZI MAJIBU CHOONI



katika utafiti uliofanywa imegundulika kuwa walimu huweka majibu vyooni ambapo wanafunzi huenda kuyachukua huko.

Pia baadhi ya walimu wasiokuwa waaminifu hutumia vitabu vya kusainia kupitisha majibu hayo kwa wanafunzi hao.

 matatizo haya mengi yamegundulika kutoka na kuhojiwa kwa maofisa elimu wa mikoa na wilaya, wanafunzi wa sekondari kukiri kuwepo kwa mambo hayo.

Na idadi kubwa ya wananchi wanaohojiwa kuhusu uelewa wa mambo hayo kuweka hadharani mambo hayo kumesaidia kugundulika kwa njia hizo mbalimbali zinazotumika kwa uvujaji wa mitihani nchini.


Hivyo basi imeshauriwa kuwa kama wewe ni msimamizi na umeanza kutilia shaka swala la watoto wengi kuomba ruhusa za kwenda chooni mara kwa mara inabidi uone namna ambavyo utaweza kufika chooni huko na ikigundulika kuwa kuna udanganyifu wa majibu huko basi haraka sana uyatolee maelezo ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua za kisheria

Na Serikali imeweka mikakati kuwa kwa yeyote atakayebainika kuwa amevujisha mitihani kwa namna moja au nyingine atachukuliwa hatua za kisheria.

No comments: