Na Joyce Mmasi( MDAU WA ELIMU)
NI majira ya saa 12 asubuhi nafika eneo ilipo Shule ya Sekondari Merembe iliyopo Manispaa ya Musoma mkoani Mara. Nia ya safari yangu ni kutaka kuzungumza na mkuu wa shule hiyo kujua pamoja na mambo mengine, mchango wa wazazi katika sekta ya elimu na ushiriki wao katika eneo hilo.
Naelekezwa moja kwa moja hadi kwa mkuu wa shule ambaye baada ya kumweleza nia ya ujio wangu, anachukua karatasi na kuniandikia ujumbe akinielekeza kumuona mwalimu wa taaluma wa shule hiyo, John Magoma.
Nikiwa ofisini kwa mwalimu huyu nashangazwa na ingia toka ya baadhi ya wanafunzi katika ofisi hiyo.Hali hii ikanisukuma kumuuliza mwalimu sababu ya wanafunzi kuingia na kutoka ofisini mwake mara kwa mara.
Jibu alilionipa likawa msingi wa mazungumzo yetu. Alijibu kwa kusema: “Hawa ni wafungwa wa nje, ni watoto walioonekana kukosa mwelekeo na kuanza kupotoka kimaadili, hivyo tunapogundua hali hii kwa mwanafunzi yoyote tunamwingiza katika utaratibu wa kifungo.”
Ukaja mfululizo wa maswali. Kwa mfano, nilimuuliza kuhusu chanzo cha mpango na mtu aliyeubuni.Mwalimu Magoma akajibu: “Mpango huu maalumu ulibuniwa na wazazi pamoja na shule katika kufuatilia kwa karibu maendeleo ya watoto...’’
Anaongeza kusema: “Wote waliopo katika mpango huu wameletwa hapa na wazazi wao baada ya kuwagundua kuanza kujiingiza katika makundi ya mitaani, kutofika shuleni, kutoroka wakati wa masomo na hata kuchelewa kufika shuleni nyakati za asubuhi.”
Kwa mujibu wa mwalimu huyo, miaka miwili ya kuwepo kwake shuleni hapo ameshuhudia ushirikiano wa karibu baina ya wazazi na uongozi wa shule katika kufuatilia maendeleo ya wanafunzi ikiwamo mabadiliko ya tabia.
Anasema kupitia mpango huo, uongozi wa shule umeandaa utaratibu ambapo wanafunzi wanaoonekana kuanza kukosa maadili, hufika ofisini kwake kila baada ya saa moja na kuweka sahihi katika kitabu maalumu kama ushahidi wa kuwepo shuleni.
“Hawa unaowaona ni wafungwa…. tumewapa jina la wafungwa wa nje… Hufika hapa kila baada ya saa moja kutia saini kuonyesha kuwa wamefika shuleni na wanaendelea kusoma na kushiriki vipindi vyote vinavyoendelea darasani ,” anabainisha.
Kinachovutia katika mpango huu wa Shule ya Mirembe siyo ubunifu tu wa kuwabana wanafunzi wanaoonekana kutozingatia masomo, bali pia ushiriki wa wazazi wanaonekana kuwa bega kwa bega na walimu katika kusimamia elimu ya watoto.
Lakini, je, mpango huo unawasaidia wanafunzi husika? Mmoja wa wafungwa waliomo katika mpango huo, Anthony Mlimila anayesoma kidato cha kwanza anakiri kukerwa na utaratibu wa kwenda kusaini ofisini kila baada ya saa moja, ingawa pia anasema kutokana na kero anayoipata amejikuta akiacha vitendo visivyofaa na kuzingatia masomo shuleni.
“Mimi nimeletwa hapa na mzazi wangu, alipofuatilia maendeleo yangu alielezwa kuwa sifiki shuleni kwa wakati na kuwa hata darasani sifiki na kumuomba mwalimu anifuatilie, na ndipo mwalimu aliponiweka katika kifungo. Nimeingia shuleni mwaka huu. Kifungo hiki cha nje kimenichosha na sikitaki tena hivyo nimeamua kusoma na kuachana na marafiki wabaya na kuzingatia masomo.”
Mwanafunzi mwingine anayesoma kidato cha pili, Zakayo Karani anasema licha ya kuwa shuleni hapo kwa miaka miwili, hakuujua mpango huo mpaka alipoingizwa korokoroni!
Naye anakiri kuwa aliyesababisha kuingia katika kifungo hicho ni mama yake anayesema aliitwa shuleni na kuelezwa namna alivyokuwa akitega masomo mara kwa mara.
Kwa upande wao, Dorry Marwa na Halima Hamisi wanaomalizia kifungo chao wanasema mpango umesaidia kubadili tabia zao mbaya ukiwamo utoro.
“Tangu niwekwe katika kifungo nimebadilika, nafika shuleni na nasoma kwa bidii, sitaki kugombana na baba yangu ambaye amekuwa akifuatilia maendeleo yangu shuleni kwa karibu na ndiye aliyeonekana kukerwa na tabia yangu na kuamua kulalamika kwa walimu ambao waliniingiza katika kifungo cha nje,’’anasema Halima huku akiungwa mkono na Dorry.
Anaongeza kusema: “ Mpango huu ulinikera na nilitaka kuachana nao na kuamua kubadilika kwa vitendo kwa kusoma na kuwa mtiifu, kuwahi shuleni, kuacha utoro na kweli mwalimu ameridhika na kunifutia kifungo. Mimi siyo mfungwa tena.”
Magoma anawasifu wazazi kwa kusema siku zote wamekuwa chachu ya maendeleo ya taaluma na maadili katika shule hiyo......“Wazazi hapa wanajitolea sana, wanachangia kwa kiasi kikubwa mipango yetu kufanikiwa.’’
Anaongeza: “ Wazazi huitikia wito tunapowaita, hushiriki vikao vya shule na hii imesaidia kwani wanafunzi wote wanaojiunga na masomo kidato cha kwanza wote humaliza shule tofauti na maeneo mengine ambayo wanafunzi wengi huachia njiani.”

No comments:
Post a Comment