Na Mdau Fredy Azzah
ZILIANZA kwa kasi na kila aina ya mbwembwe. Wazazi wengi waliojaaliwa kipato walizichangamkia kwa kuwapeleka watoto wao.Baadaye hata wazazi wa kipato cha chini na kile cha kubahatisha nao hawakusita kudunduliza alimradi watoto wao nao wasome katika shule zilizopewa jina la ‘Shule za Kimataifa’
Shule hizi zilizoanzishwa kama uyoga mwanzoni mwa miaka ya 2000 zikawa mshindani mkubwa wa shule za Serikali na zile binafsi za kawaida.Kwa watu wengi Iliaminika hizi ndizo shule zilizokuwa zikitoa elimu bora, huku kigezo kikubwa kikiwa uwezo wa wanafunzi wake kutumia lugha ya Kiingereza kilichotumika kama chambo cha kuwavutia wateja.
Ukitoa matumizi ya Kiingereza kama lugha ya kufundishia, uzuri wa miundombinu, usafiri na utoaji chakula kwa wanafunzi vinatajwa kuwa vichocheo vingine vikubwa vilivyowavuta wazazi wengi.
Hata hivyo, mwongo mmoja baadaye baadhi ya watu wanasema shule hizo na hata zile zinazojulikana Kiingereza kwa majina ya Academy, English Medium zimeanza kupoteza umaarufu kwa wazazi wengi.
Ofisa Mipango wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TenMet), Anthony Mwakibinga anaeleza kuwa miongoni mwa sababu kubwa za kushuka kwa umaarufu wa shule za kimataifa na zile za mchepuo wa Kiingereza ni kuwapo kwa shule nyingi za aina hiyo huku zingine zikikosa sifa hasa kwa kuwa na walimu wasiokuwa na sifa.
Anasema mara nyingi kigezo cha ualimu mzuri kinachotumiwa na wamiliki wa shule hizi ni kujua Kiingereza na ndiyo maana wamekuwa wakiwatumia raia wa nchi jirani wanaowaamini kuwa na ujuzi mkubwa wa lugha hiyo.
“..... kigezo chao wanaangalia kujua Kiingereza, hii nayo imechangia sana kuzishusha. Ualimu ni taaluma siyo kila mtu tu anaweza kufundisha,” anasema Mwakibinga na kuongeza:
“Sababu nyingine ni kuwa, baadhi ya hizi shule ni za kitapeli, wazazi wakiwapeleka watoto wao, hawaendi kupata kile walichotarajia.’’
Pamoja na udhaifu huu, Mwakibinga anasema, shule hizi zina unafuu ikilinganishwa na shule za Serikali.... “Walimu wa hizi shule wanalipwa vizuri, wanaingia darasani kufundisha na pia wanawasimamia watoto vizuri. Huwezi ukasema kuwa sasa shule za Serikali ni bora kuliko hizi.”
Juma Abdala anayesomesha mtoto wake katika shule moja ya kimataifa ambayo hakutaka itajwe gazetini, anasema amepoteza kiasi kikubwa cha fedha kumsomesha mwanawe katika shule zaidi ya mbili bila ya mafanikio yoyote kitaaluma.Kwake , shule hizi zimeshindwa kukidhi matarajio yake.

“Shule anayosoma mtoto wangu sasa ni ya tatu, zote alizokuwa mwanzo nilimhamisha. Mtu unalipa fedha kibao za ada lakini hakuna cha zaidi unachokiona zaidi ya mtoto kurudi usiku amechoka kutokana na kuzunguka na gari la shule,” anaeleza.
Anasema alichogundua kuhusu shule hizi ni kuwa watoto wanafundishwa mambo makubwa kitaaluma na weledi wa lugha ya Kiingereza
Anasema alichogundua kuhusu shule hizi ni kuwa watoto wanafundishwa mambo makubwa kitaaluma na weledi wa lugha ya Kiingereza
“Mwishowe inabidi tu umpeleke mtoto huko huko kwa sababu huko serikalini ndiko hakufai kabisa. Zile shule ambazo mtoto wako anaweza kupata elimu ile unayoitaka, ada yake ni kubwa sana, hatimaye tunamuomba Mungu tu awaongoze watoto wetu,” anaongeza kusema.
Kwa upande wake, Lilian Joseph anayefundisha katia moja ya shule za mchepuo wa Kiingereza mkoani Arusha anasema shule hizo zimepungua mvuto kwa wazazi wengi waliobaini kuwa elimu siyo kujua lugha ya Kiingereza pekee.
Kwa mtazamo wake, haamini kama shule hizo pekee ndizo zinazotoa elimu bora kuliko nyingine…..” Labda uniambie hicho Kiingereza, kidogo naweza kukukubalia, lakini elimu siyo Kiingereza na hili ndilo kosa wanalofanya wazazi wengi.

Arnold Samuel ni mmoja wa watu waliosoma katika shule za mchepuo wa Kingereza. Anasema elimu inayotolewa huko bado ni bora ikilinganishwa na shule za Serikali.
“Tangu nikiwa darasa la kwanza, nimekuwa nikisoma Engilish Medium (shule za mchepuo wa Kiingereza), kusema kuwa eti katika shule hizi hakuna kitu wanafunzi wanachopata zaidi ya kujua Kingereza, ni kusema ovyo bila kuwa na hata chembe ya utafiti wala taarifa za ukweli,’’anaeleza.
Samuel ambaye kwa sasa ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam anasema ufundishaji katika shule hizo ni wa hali ya juu huku ukichagizwa na matumizi ya vifaa vya kufundishia na kujifunzia jambo analosema linakosekana katika shule za Serikali.
Pia anapinga kuporomoka kwa umaarufu wa shule hizo kwa kusema: “Siku hizi hata muuza genge anaweza kujichanga na kumpeleka mtoto wake katika shule hizi. Zamani watu waliokuwa wakiwapeleka watoto huko ni wale waliokuwa wanaonekana ni matajiri sana, hali hii ndiyo inayofanya watu waseme umaarufu wa hizi shule umeshuka.
No comments:
Post a Comment