Na Mdau Joyce Mmasi
VIONGOZI wa Serikali na wale wa kisiasa ndio wanataotarajiwa kuwa chachu ya kuleta maendeleo hususan katika kuhamasisha jamii kusaidia kukuza sekta mbalimbali ikiwamo elimu.
Hata hivyo, katika hali ambayo ni kinyume na matarajio ya wengi wanasiasa na viongozi serikalini wanatajwa kuwa vinara wa kukwaza maendeleo ya jamii hasa katika uwanja wa elimu.
Hivi ndivyo hali ilivyo katika Wilaya ya Musoma Mjini ambako viongozi wanaosimamia sekta ya elimu wanasema pamoja na kuwepo kwa mwitiko mkubwa wa jamii kuchangia elimu, matamshi ya wanasiasa na viongozi wa Serikali yanachangia kurudisha nyuma juhudi hizo.
“Wazazi wamejitokeza kwa wingi katika kuchangia sekta ya elimu, ukiangalia ujenzi wa shule za kata, ongezeko la idadi ya wanafunzi na hata kuhamasisha watoto wao kwenda shule……lakini tofauti na mikoa mingine hapa Musoma tatizo huja katika kutoa michango ya pesa ambapo wazazi wengi ni kama wamekataa kujitolea, ” anasema Ofisa Elimu wa Sekondari wa wilaya hiyo, Jackob Makala.
Anasema hatua hiyo ya wazazi kukataa kuchangia inatokana na kauli mbalimbali za viongozi hasa wale wa kisiasa ambao wamekuwa wakitafuta uungwaji mkono kwa kueleza kuwa suala la gharama zote zinazohitajika katika elimu ya mtoto ni jukumu la Serikali pekee.
Makalla anaeleza kuwa hali hiyo imekwamisha juhudi za Serikali kuwataka wananchi wajitolee kusaidia elimu ya watoto wao, kwani wazazi wengi wameamua kuitikia wito wa wanasiasa wanaowakataza kutoa michango.
“Kwa mfano,, mimi nimetoka Igunga, kule tulikuwa tumeweka utaratibu mzuri na kwa kweli tulifanikiwa sana, kwamba mbali na ada ya shilingi 20,000, mzazi alipaswa kutoa mchango mwingine wa shilingi 10,000, anasema na kuongeza;
“…. kule wazazi walikuwa wanakaa na kuazimia kuchangia zaidi ya kiasi hicho kilichopangwa na Serikali ili kusaidia katika masuala mengine yakiwemo malipo ya walimu wa muda ambao huchukuliwa ili kusaidia kufundisha kwa kuwa shule nyingi zina idadi ndogo ya walimu.”
Aidha, Makalla anasema utaratibu wa wazazi kutoa michango ya nyongeza mbali na ile iliyopangwa na wizara, hufanyika katika mikoa mbalimbali Tanzania ukiwemo mkoa wa Tabora hasa wilaya ya Igunga ambako anasema wazazi wa kila shule hujiwekea utaratibu wa kiasi cha nyongeza kulingana na uwezo wao ili kusaidia sekta hiyo.
Kwa mkoani Mara ambako wananchi wameamua kuwasikiliza wananchi, anatoa mfano wa Shule ya Sekondari ya Musoma anayosema kiango cha taalumu kimepungua kwa sababu ya ukosefu wa walimu ambao huenda idadi yao ingeongezeka kama wazazi wangeshiriki kikamilifu kutatua kero zinazoikabili shule hiyo.
“Pale Musoma Sekondari idadi ya walimu waliopo ni chini ya 30 lakini walimu wanaohitajika kulingana na idadi ya wanafunzi waliopo ni 70. Sasa utaona ilivyo ngumu kwa wanafunzi wa pale kufaulu katika kiwango kinachostahili……hii ni kwa shule karibia zote zilizopo Manispaa ya Musoma,” anasema.
Anaeleza kuwa asilimia 90 ya wazazi wanapinga kutoa michango yoyote katika shule na kusema hali hii imeongezeka zaidi miaka miwili iliyopita kutokana na manispaa hiyo kuongozwa na chama cha upinzani cha Chadema.
Kwa upande wake, Kaimu Ofisa Elimu wa manispaa hiyo anayeshughulikia elimu ya msingi, Erasto Mhina anasema mwitikio wa wazazi upande wa elimu ya msingi katika manispaa hiyo ni mkubwa kwani wazazi wengi wanajitokeza kuandikisha watoto wao. Anasema zaidi ya asilimia 95 ya watoto wenye umri wa kwenda shule wanaandikishwa kujiunga katika shule za msingi.
Hata hivyo pamoja na mwamko huu, Mhina anaeleza bado wanakumbana na changamoto mbalimbali ikiwamo wazazi kujitoa kufuatilia elimu ya watoto wao na kususia michango ya maendeleo ya elimu.

No comments:
Post a Comment