Esther Mwimbula, Morogoro
SERIKALI inatarajia kutumia Sh202,202,390,986 kuboresha vyuo 55 vya maendeleo ya jamii (FDCs) nchini, viweze kukidhi viwango na sifa kwa ajili ya kuanza kutoa mafunzo ya ufundi stadi, lengo likiwa ni kutoa nafasi kwa vijana wengi kupafa nafasi za mafunzo.
Akizungumza kwenye mahafali ya wahitimu wa ualimu wa mafunzo ya ufundi ngazi ya stashahada na cheti katika Chuo cha Ualimu wa Ufundi Stadi (Veta), Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa, alisema awamu ya kwanza ya mradi huo itahusisha vyuo 25 vya maendeleo ya wananchi.
Dk Kawambwa alisema awamu hiyo itagharimu Sh67,400,799,662 na awamu ya pili na tatu ya mradi itahusu vyuo 15 na kila moja itagharimu Sh67,400,799,662 na kwamba, ukamilikaji wake utasaidia vijana wengi kujiunga na kunufaika na mafunzo ya ufundi stadi.
Alisema mpango huo umetokana baada ya kutambua umuhimu wa mafunzo ya ufundi stadi nchini katika kuongeza fursa kwa vijana kujiunga na mafunzo hayo, sambamba na ujenzi wa vyuo vya ufundi vya wilaya za Lindi, Pwani, Manyara na Chuo cha Teknolojia ya Habari cha Dar es Salaam vitakavyokamilika ujenzi wake Januari mwakani.
Waziri Kawambwa alisema Benki ya Maendeleo Afrika (ADB), itasaidia ujenzi wa chuo cha mambo ya hoteli na utalii ambacho ujenzi wake unakadiriwa kukamilika karibuni na kuanza kuchukua wanafunzi Januari mwakani.
Dk Kawambwa alisema mipango mingine ya Serikali iliyojiwekea, ni kupanua na kuinua ubora wa elimu ya ufundi stadi, uandaaji na utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya elimu hiyo nchini.
Alibainisha kuwa elimu ya ufundi stadi katika karne ya sayansi na teknolojia ina mchango mkubwa katika kuleta maendeleo haraka, huku ikiwezesha wahitimu wa vyuo hivyo kuwa mahiri, wabunifu na wenye ari kwenye utendaji kazi.
CHANZO (MWANANCHI)

No comments:
Post a Comment