Thursday, November 17, 2011

MWALIMU WA SEKONDARI AOMBA RUSHWA YA NGONO KWA MWANAFUNZI WA KIDATO CAHA KWANZA

Na Francis Godwin, Iringa
Hii ni aibu nzito kwa Mchungaji Michael Ngilangwa (35) ambaye pia ni mwalimu wa Shule ya Sekondari Pomerin, Wilayani Kilolo, Mkoani Iringa kupandishwa kizimbani mwishoni mwa wiki iliyopita akituhumiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuomba rushwa ya ngono kutoka kwa mwanafunzi wa kidato cha kwanza ili amsaidie kujua somo la Kiingereza.

Mchungaji huyo wa roho za watu alijikuta akikwea kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Iringa na kusimamishwa mbele ya Hakimu Martha Ngaze ambapo mwendesha mashitaka wa Takukuru mkoani hapa, Imani Nitume alisema Ngilangwa ni mwajiriwa wa shule hiyo inayomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa.
Alidaiwa kuwa, pamoja na kuomba rushwa ya ngono Ngilangwa anatuhumiwa kutaka kumbaka mwanafunzi huyo (Jina linahifadhiwa kwa sababu za kimaadili), mwenye umri wa miaka 14, hivyo kosa hilo kuwa la pili.

Mwendesha mashitaka Nitume aliongeza kusema kuwa, Mchungaji Ngilangwa anashitakiwa kwa kuvunja kifungu cha 25 cha sheria namba 11 ya mwaka 2007 ya kuzuia na kupambana na rushwa katika tukio hilo lililotokea  katika Nyumba ya Kulala Wageni ya Mianzini mjini Iringa.
Alidai kuwa, Mchungaji Ngilangwa akiwa na mwanafunzi huyo ndani ya nyumba hiyo ya wageni, aliomba rushwa ya ngono kutoka kwa denti huyo kwa ahadi atamsaidia somo la Kiingereza na Biblia pamoja na kumpatia mahitaji yake mengine madogo madogo awapo shuleni hapo.

chanzo,  global publishers 

No comments: