Katika kuadhimisha miaka 50 ya Tanzania Bara ,Serikali imeandaa shindano la Insha
litakalowashirikisha wanafunzi wa Ngazi zote za Elimu .
Mada ya Insha hiyo ni
“TATHMINI YA MAENDELEO YA HUDUMA ZA JAMII,HALI YA UCHUMI
WA NCHI NA UTAWALA BORA KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA
UHURU WA TANZANIA BARA.”
Matarajio kwa Washiriki ni
• Kuchambua mafanikio na changamoto katika sekta za Elimu, Afya, Maji, Uchumi,
Biashara na Utawala katika kipindi hicho cha miaka 50 ya Uhuru
• Kuelezea mchango wa Shule/Chuo cha Mshiriki katika kuleta maendeleo katika/
kwenye maeneo hayo
• Kubainisha wadau waliotoa mchango mkubwa wa kimaendeleo katika maeneo/sekta
tajwa
Namna ya Kushiriki:
• Insha ya wanafunzi wa Shule za Msingi zinatarajiwa kuwa na urefu wa maneno
kati ya 700-1200 wakati zile za wanafunzi wa sekondari zitakuwa na urefu wa
maneno kati ya 1000-1500
• Maudhui ya Insha yaoneshe jinsi shule zinavyoweza kuhusika katika kuleta
maendeleo ya jamiii
• Kila shule itakayoshiriki itachagua Insha bora mbili kutoka shule yao na kuziwasilisha kwa Afisaelimu wa Halmashauri (Msingi na Sekondari),
• Halmashauri nao watajipanga kupata Insha 5 bora za Msingi na 5 bora za sekondari na
kuziwasilisha kwa Afisaelimu wa Mkoa.
• Mkoa nao utajipanga kupata Insha 2 bora za Msingi na 2 bora za Sekondari kutoka Mkoa
wao.
• Insha zitakazowasilishwa ziwe zimeandikwa kwa mkono wa Mshiriki mwenyewe
• Insha zitakazochaguliwa katika ngazi ya mkoa ziwasilishwe Wizara ya Elimu na Mafunzo
ya Ufundi kabla ya tarehe 27/11/2011.
Insha Bora Ki-Taifa
• Insha 3 bora kutoka Shule za Msingi,
• Insha 3 bora kutoka Shule za Sekondari,
• Insha 3 bora kutoka Vyuo na Vyuo Vikuu
Zawadi za Washindi
• Shilling million 18 zitatolewa kwa Washindi wa Insha na Shule/Vyuo vyao. Aidha Insha
zitakazofika ngazi ya Taifa zitachapwa katika magazeti na / au toleo maalum la Insha za Miaka 50 ya Uhuru,
• Washiriki 9 bora kitaifa watapokea zawadi zao siku ya kilele cha Miaka 50 ya Uhuru
• Washindi wengine katika ngazi ya Mikoa na Halmashauri watapata vyeti na zawadi zitakazotolewa katika ngazi hizo
No comments:
Post a Comment