Wednesday, November 30, 2011

MAMA LAMBETA MAHAI AIELEZEA TAASISI YA ELIMU YA WATU WAZIMA


                   MKURUGENZI WA ELIMU YA WATU WAZIMA MAMA LAMBETA MAHAI
                      AKIWA NA AFISA WA UBALOZI WA SWEDEN ANAYESHUGHULIKIA
                                                  ELIMU NDUGU ARVIDSON STELLAN

 Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima ilianzishwa mwaka 1960 kama sehemu ya kitengo cha mafunzo ya ziada cha Chuo Kikuu kishiriki cha Makerere Kampala, Uganda ambacho kilikuwa chini ya Chuo Kikuu cha London, Uingereza.
Mwaka 1963 taasisi  ikawa chini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kama idara ya elimu ya watu wazima. Tasisi hiyo iliendelea kukua na kupata hadhi ya kuwa shirika la umma linalojitegemea na kutoa huduma nchini chini ya Sheria ya Bunge Na 12 ya mwaka 1975.
Malengo ya taasisi hii ni pamoja na kutoa mafunzo ya elimu ya watu wazima na maendeleo ya jamii kwa watalaam na waendeshaji wa elimu ya watu wazima, kutoa elimu ya ana kwa ana na masafa pamoja na kufanya utafiti wa elimu ya watu wazima.
Malengo mengine ni kutoa ushauri kwa Serikali na asasi nyingine kuhusu elimu ya watu wazima, kutoa elimu kwa umma kuhusu masuala  mtambuka kama afya, umasikini na kuandaa mitaala, majarida, vitabu vya elimu ya watu wazima na moduli za elimu masafa.

No comments: