Mkoa
wa Dar es Salaam umetoa matokeo yake ya waliohitimu darasa la saba
mwaka huu ambapo shule ya Tusiime ya Tabata jijini Dar es Salaam
imeongoza kwa Mkoa mzima wa Dar es Salam na katika Wilaya ya Ilala.
Shule hiyo ndiyo imekuwa ikiongoza matokeo ya mkoa na Wilaya ya Ilala tangu mwaka 2005.
Katika matokeo hayo wanafunzi kumi bora wa kike waliofanya vizuri wanatoka shule ya Tusiime na wavulana walioingia kumi bora saba wanatoka shule hiyo.
Akitangaza matokeo hayo katika ofisi ya mkoa jana, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mbando akiwa na Ofisa Elimu wa Mkoa, Raymond Mapunda, aliwataja wanafunzi kumi bora wa kike kuwa ni Janeth Kijazi aliyepata alama 234 (Tusiime), Justina Kalalaa 234 (Tusiime), Kellen Mudogo 234 (Tusiime), Thecla Ngewe 231 (Tusiime), Stella Kagumila 230 (Tusiime), Asia Komba 229 (Tusiime), Grace Nyondo 226 (Tusiime), Praise Bagenda 226 (Tusiime), Lisa Magoti 225 (Tusiime) na Najima Majid 224 (Tusiime).
Kumi bora waliofanya vizuri kwa upande wa wavulana ni Jimmy Luhomvya 233 (Tusiime), Dule Mutagwaba 231 (Tusiime), Fray Seyumwe 231 (Tusiime), Maximillian Machage 229 Moga Kinondni, Saad Mussa 229 (Tusiime), Gerald Kasamala 229 (Tusiime), Gift Kilupa 229 (Tusiime).
Wengine ni Joel Mutagwaba 228 (Tusiime), Shaban Kawaia 227 Mtoni Temeke na Alfred Shami wa shule ya msingi Mlimani.
Katibu tawala alisema waliofanya mitihani wa kumaliza la saba mwaka huu walikuwa 58,093 na waliofaulu mtihani huo ni 51,433 sawa na asilimia 88.5 na waliochaguliwa kujiunga na shule mbalimbali za sekondari ni 39,681.
Alisema wanafunzi waliofaulu mitihani ya kumaliza la saba mwaka 2011 walikuwa asilimia 79 wakati mwaka huu ni asilimia 88 hivyo ufaulu umeongezeka kwa asilimia 10.
Akizungumzia matokeo hayo, Ofisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda aliipongeza shule ya Tusiime kwa kufaulisha wanafunzi wengi zaidi na kwa alama za juu.
“Walimu waliofanikisha wanafunzi hawa kufanya vizuri naomba wataambuliwe na uongozi ikiwezekana wapewe motisha na naomba manispaa ya Ilala nayo iwatambue kwa kufanya vizuri zaidi ili iwe motisha kwa wengine,” alisema Mapunda.

CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment