Sunday, December 18, 2011

TUNAWEZA KUJIGAMBA UFAULU WA HESABU UMEONGEZEKA KWA MASWALI YA A B C D?

JAMANI nomba mnisamehe kama nitakuwa nimekosea ila napata tabu sana klama mdau wa kawaida kabisa wa elimu kuona watu wakisimama kwenye vyombo vya habari na kusema kuwa ufaulu wa hesabu umeongezeka sana il hali mtihani huu ulifanywa kwa mtindo wa kuchagua jibu sahihi (multiple choice) kutoka swali la kwanza mpaka la mwisho.

kutokana na upeo wa akili yangu ulivyo mdogo na mawazo yangu fnyu naona hii sio sawa kabisaa, hii ni sawa na kupiga ngoma kwa kutumia pamba, kwa mtu mwenye akili na ajaribu kutafakari ni vipi hapa vipimo vitakwenda sawa kwa utaratibu huu?

mimi naona kuwa walimu ni wakati wetu umefika tujenge baraza la kuishauri serikali namna ambavyo mitihani hii inatakiwa iwe kutokana na uhalisia wa namna tunavyofundisha ni hatari sana kama tutaendelea na utaratibu huu kwa miaka angalau mitano tu ijayo kielimu tutakuwa chini kuliko tunavyofikiri,

kwenye suala la uchakachuaji naomba kuishauri serikali kuwa kwenye suala zima la upimaji wa mtoto cheti kisiwe kigezo bali watu waangalie namna ambavyo maendeleo yake mtoto huyo kibinafsi ili kupata kujua ukweli wa utambuzi binafsi wa mtoto huyo. serikali isiogope kuwekeza kiukweli kwenye wasimamizi waadilifu na wawalipe vizuri kuepusha mianya ya rushwa kwa kiasi fulani.

nimejaribu kuangalia nchi nyingi wenzetu wamefanikiwa kutokana na utaratibu huu na hivyo kufanya wenzetru wengi kupiga hatua sana kielimu sasa tunawaomba serikali pamoja na mambo mengine wawashirikishe wadau na wasomi mbalimbali kwani ugumu unaoonekana sasa hivi ni kuwa serikali wajue kuwa wanaowaongoza ni wasomi hivyo ni ngumu sana kuwapeleka kisiasa namna ambavyo wanafikiri wao kama ilivyokuwa zamani.

ZAMA ZA SIASA ZIMEKWISHA, HIZI NI ZAMA ZA UTENDAJI JAMANI

No comments: