MATOKEO ya mitihani wa Taifa wa darasa la saba, yanaonyesha kuongezeka kwa kiwango cha ufaulu kwa somo la Hisabati kwa asilimia 14
Ufaulu huo umeongezeka kwa tofauti ya matokeo ya mwaka jana ambapo ufaulu huo kutoka asilimia 24.70 mwaka jana hadi asilimia 39.36 kwa mwaka huu.
Matokeo hayo yalitangazwa jana jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philip Mulugo
Naibu huyo alisema idadi ya ufaulu kwa mwaka huu inaridhisha tofauti na mwaka jana, ambapo kiwango cha ufaulu kwa masomo ya Sayansi, Hisabati na Kiingereza kimeongezeka .
Alibainisha kuwa jumla ya wanafunzi 983,545 walifanya mitihani na kati ya hao 567,567 wamefaulu na wamechaguliwa kuingia kidato cha kwanza mwaka kesho.
Alifafanua kuwa, wanafunzi 515,187 sawa na asilimia 90 waliofaulu wamechaguliwa kuingia kidato cha kwanza katika shule za sekondari za serikali
Aidha alisema wizara hiyo imewafutia matokeo jumla ya watahiniwa 9,736 baada ya kubainika kuwa walifanya udanganyifu katika mitihani hiyo kati yao wavulana ni 4,943 na wasichana ni 4,793.

No comments:
Post a Comment