Friday, November 4, 2011

WANAWAKE WACHANGAMKIE ELIMU YA MASAFA - Mh.Mizengo Pinda


Na mdau wa blog hii sumbawanga.
Takwimu za Kitaifa za Chuo Kikuu Huria zinaonesha kuwa, hadi  sasa  Wanaume  ndio  wanaochangamkia  sana fursa ya  kuwepo  kwa  Chuo  hiki kwa wingi kuliko Wanawake. Kwa mfano, mwaka 2007/2008 Wanawake waliokuwa wamedahiliwa na Chuo Kikuu Huria walikuwa Asilimia 23 tu kati ya Wanafunzi 19,909 walikuwa wamedahiliwa na mwaka 2010/2011 Wanawake walikuwa Asilimia 30 ya Wanafunzi 44,272 waliodahiliwa.
Vilevile, Takwimu za Udahili katika Kituo hiki zinaonesha kuwa katika kipindi cha miaka 10 iliyopita (mwaka 2001 na 2010) Kituo hiki kilidahili Wanafunzi 886. Kati yao, Wanaume walikuwa 685 sawa na Asilimia 78 na Wanawake walikuwa 189 sawa na Asilimia 22 tu ya Wanafunzi wote waliodahiliwa.
Ibara ya 85(e)(v) ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi 2010 – 2015 inaielekeza Serikali Kuongeza idadi ya Wanafunzi wa Kike katika Vyuo Vikuu ili ifikie angalau Asilimia 40 ya Wanavyuo wanaodahiliwa kila mwaka. Ikiwa Wanawake wataongeza bidii ya kutumia fursa zilizopo hususan za kuwepo kwa Vyuo vinavyotoa Elimu kwa njia ya Masafa kama Chuo Kikuu Huria, lengo hili linaweza kufikiwa haraka. Napenda kutumia fursa hii kuwahimiza Wanawake kutumia fursa hii ya Elimu ambayo inamwezesha Mwanamke kupata elimu wakati akiendelea na majukumu yake kwa Familia na Taifa.

No comments: