Thursday, November 10, 2011

WALIMU KULIPWA MALIMBIKIZO YAO YOTE KABLA YA KRISMAS

NA MDAU WA ELIMU

Leon Bahati
BAADA ya kubanwa na Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Serikali sasa imeahidi kuanza kuwalipa walimu malimbikizo ya madai yao ya muda mrefu yanayofikia Sh49.24 bilioni.Malipo hayo ni makubwa yakilinganishwa na madai ya awali ya Sh48.6 bilioni ambayo CWT iliyawasilisha kwa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, kisha ikayapuuza na kusema siyo ya ukweli.

Lakini baada ya mazungumzo yaliyodumu kwa miezi mitatu kati ya Serikali na CWT, imeazimiwa kuwa madai hayo ya walimu zaidi ya 75,000 yalipwe kwa mkupuo mwezi huu au kwa awamu mbili, ya mwisho ikamilishwe Desemba mwaka huu.

Akizungumzia makubaliano hayo Dar es Salaam jana ikiwa ni siku moja baada ya kumalizika mazungumzo hayo, Rais wa CTW, Gratian Mukoba alisema: “Kwa hiyo, walimu nawataka wajiandae kula Krismasi kwa furaha.”
Hata hivyo, Mukoba alionya kwamba iwapo Serikali itakiuka makubaliano hayo, Baraza Kuu la CWT litakalofanyika mwezi ujao litaamua hatua za kuchukua.

Maazimio ya majadiliano
Baada ya Serikali kupokea na kuhakiki vielelezo mbalimbali vilivyowasilishwa kwake na CWT, Mukoba alisema vilibainika kuwa ni sahihi na ziada ya Sh5.9 bilioni.

“Serikali imekubali kuwa walimu wanadai Sh49.24 bilioni baada ya taarifa ya uhakiki kukamilishwa,” alisema Mukoba na kutoa mchanganuo:
“Kati ya fedha hizo, Sh5.9 bilioni ni kwa wakufunzi wa vyuo vya walimu, wakaguzi, walimu wa mazoezi na wa sekondari waliokuwa na madai yao kabla ya ughatuaji. Walimu zaidi ya 5,500 wanahusika.”

Mukoba alisema uchambuzi wa kina unaonyesha kwamba, zaidi ya Sh25 bilioni ni madai yanayotokana na malimbikizo ya mishahara.
“Tangu CWT iwasilishe madai ya Sh48 bilioni, Serikali imekwishalipa Sh6 bilioni kama malimbikizo ya walimu. Hii inatupa picha kuwa wasingekuwa wamelipa kiasi hicho, madai yangeongezeka na kufikia Sh54 bilioni,” alisema na kuongeza:

“Serikali imepokea ushauri wa CWT wa kulipa madeni yote… kwa awamu moja Novemba (mwezi huu) au kwa awamu mbili, kati ya Novemba na Desemba (mwaka huu).”

Alisema kwenye makubaliano hayo wameamua malipo ya awali yatokane na madai ya madaraja, ambayo ndiyo kilio kikubwa cha walimu.
Kutokana na makubaliano hayo, Mukoba alisema Serikali imeahidi kutoa orodha ya walimu pamoja na viwango vya malipo yao Novemba 18, mwaka huu.
Ufisadi wa Halmashauri
Katika kuhakiki malipo ya walimu, Mukoba alisema wamegundua madudu mengi yanayofanywa na baadhi ya Halmashauri nchini.“Upo ushahidi kuwa baadhi ya walimu waliohakikiwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mwaka 2009 wanadai tena,” alisema Mkoba akitoa sababu mbili:

“Fedha zilizohakikiwa na kutumwa kwenye halmashauri hazikuwafikia walimu husika. Kesi kama hii inawahusu walimu 194 wa Wilaya ya Ilala ambao zaidi ya Sh200 milioni hazikuwafikia.”

“Baadhi ya walimu (halmashauri mbalimbali nchini) hawakulipwa kiasi chote kilichopitishwa na CAG. Kwa mfano, mwalimu aliyepitishiwa malipo ya Sh500,000 alilipwa Sh50,000 tu.”

Chimbuko la mgogoro
Walimu kupitia CWT wamekuwa wakivutana na Serikali kuhusu madai yao kwa miaka mitatu sasa. Mara kadhaa ndani ya kipindi hicho, wamekuwa wakitishia kufanya mgomo wa walimu nchi nzima.Katika kikao cha Baraza la CWT Julai mwaka huu, menejimenti ya chama iliagizwa kutoa notisi kwa Katibu Mkuu wa Utumishi na Menejimenti ya Umma kutangaza mgogoro na Serikali.

Katibu Mkuu wa Utumishi, George Yambesi aliamua kuunda kamati ya majadiliano na CWT ili kutatua mgogoro huo ikiwa ni pamoja na kuhakiki madai ya walimu.“Kimsingi vikao hivi viliendeshwa kwa ushirikiano wa pande zote mbili, japokuwa Serikali ilikuwa inaamini kuwa taarifa za CWT si sahihi,” alisema Mukoba.

Waraka kandamizi
Mbali na madai ya malimbikizo hayo, CWT imekuwa ikiibana Serikali ikitaka itatue tatizo la kutowapandisha walimu madaraja kulingana na sifa zao, kutowalipa kulingana na madaraja na kuwapo na waraka kandamizi dhidi ya walimu.

Mukoba alisema Serikali imeiomba CWT iiongezee tena kipindi cha mwezi mmoja, ambao unamalizika Novemba, mwaka huu ili kutoa taarifa juu ya namna ilivyoshughulikia waraka kandamizi unaolalamikiwa na walimu ikiwa ni pamoja na kuufuta.

Waraka huo uliotolewa mwaka 2009, alisema unawalenga walimu ambao wamekuwa wakijiendeleza ili wawe na uwezo zaidi wa kumudu kazi zao za kufundisha.

“Kwa mujibu wa waraka huo, walimu waliojiendeleza Serikali huwarudisha nyuma kwenye ngazi za mshahara ambazo walishazipita,” alisema Mukoba na kuongeza: “Waraka huo unachukuliwa na walimu na CWT kuwa umelenga katika kuwakatisha tamaa walimu wasijiendeleze.”

Yambesi hakupatikana jana kufafanua juu ya mkakati wa kutekeleza makubaliano hayo, baada ya kuripotiwa kuwe kwenye vikao.

No comments: