Jana ilikuwa siku nzuri sana kwa wafungwa wa kenya baada ya kufanya mtihani wao wa kumaliza darasa la nane, kama ilivyo adda kila inapofika mwezi wa kumi na moja wanafunzi wa shule ya msingi huungana na wenzao wote nchini humo kufanya mtihani huo muhimu kwa safari ya kielimu.
Aidha suala hilo limeonekana kuwa ni la kushangaza kwa baadhi ya wananchi wa Tanzania ambao walipata fursa ya kuongea na blog hii na kusema kuwa huo ni mfano mzuri sana kwa nchi yetu ya Tanzania kama tunataka kweli kutimiza elimu yenye usawa kwa kila raia kwani hata wafungwa wana haki ya kupata elimu.
Bwana Iddy Kiffile ambae ni mwalimu wa shule moja ya sekondari iliyopo wilaya ya pwani pale kibaha anasema hakuwahi kusikia hata mara moja wafungwa katika nchi yetu wakipewa nafasi hiyo adhimu ambayo ni muhimu sana kwao kwani muda mara nyingi huwa ahungoji mtu.
Alisema kuwa watu wengi hudhani wafungwa wanapokuwa wapo gerezani huwa ndio wamepoteza haki zao zote huku uraiani hususani za kimasomo na haki hizo hurudi pindi tu watakapokuwa huru. Hii si kweli kabisa kwani tumeshuhudia kutoka nnchi za wenzetu huko nje watu mbalimbali wakipata mpaka masters ikiwa wapo magerezani na wengine huzindua vitabu mbalimbali kwakuwa wanapata misaada ya kutosha na nafasi na hii hutokana na nchi husika kujali maslahi ya wananchi wao hususani kwenye suala zima la elimu.
Naye bwana ayoub bwanamadi ambaye ni mdau wa elimu aliyehamia morogoro akitokea Tanga alitoa wazo kuwa huu ni wakati muafaka kwa serikali kuona umuhimu wa watu hawa na kuona namna ambavyo wanaweza kuwasaidia ili waweze kupata elimu na pindi wanapotoka tu magerezani waweze kutumia elimu walizopata ili kujenga taifa lao
No comments:
Post a Comment