Tuesday, November 29, 2011

KAMA NINGEWEZA NINGESHAURI TUSISHEREHEKEE MIAKA 50 YA UHURU KIELIMU

   
Na Mwanamapinduzi.
Kwa maoni na fikra zangu  nimefikiria mambo mengi sana juu ya sherehe kubwa sana ambayo ipo mbele yetu ambayo kwa namna moja ama nyingine inatushughulisha sana na kuyaacha kabisa yale mambo ambayo ni ya muhimu sana kuliko tunavyodhani KIELIMU.
    Maandalizi haya yanajaribu kugusa sehemu kubwa sana ya matumizi ambayo kama tungeyatumia kwa manufaa zaidi yangesaidia mpaka miaka hata ishirini ijayo KIELIMU, nasema hivi kwasababu kila ninachokiona nashindwa kukielewa kama ni sawa au vp? kwa kuwa malalamiko yamekuwa ni mengi kuliko uwezeshwaji.
malalamiko hayo yamegusa kwenye nyanja zifuatazo:-
- Asilimia kubwa ya walimu wa Tanzania wamekuwa walimu baada kukosa nafasi sehemu nyingine.
- Wanafunzi wengi wa shule za msingi wanakaa chini na wengine chini ya miti.
- Walimu wachache waliopo hawana maslahi ya kutosha hivyo wamekata tamaa.
- Asilimia kubwa ya walimu ni wale waliofaulu viwango wa chini sana kwenye elimu ya sekondari.
- Idadi kubwa ya wanafunzi darasani kuliko uwezo wa darasa.
- Shule kukosa nyumba za walimu.
- Kutokuwa na bodi ya walimu.
- Mtihani shule za msingi kuwa na maswali ya kuchagua tu(multiple choice) mpake hesabu.

- Hakuna chakula cha mchana mashuleni.
- Migomo inaongezeka kila kukicha.
- Shule kukosa vifaa vya kisayansi na maabara.
- Baadhi ya walimu wakuu kutumia madaraka yao kwa maslahi yao.
- Malengo ya MMEM na MMES ya kwanza kutofanikiwa.
Kwa haya na mengine mengi nahisi naogopa kukubali kusherehekea siku hii kwa kuwa bado hatuna haja ya kufurahia kielimu kwani miaka hii imekuwa na changamoto badala yake tunahitaji kuhuzunika kwa kuwa bado hatujafikia lengo tulilolihitaji na tulilojiwekea kwa kuwa nahisi baadhi ya watu bado ni wajinga, wana maradhi mengi na masikini sana hivyo bado tunaendelea kuliwa na na maadui wetu hawa

Maoni haya ni yangu binafsi kutokana na upeo wa elimu yangu
mawasiliano  0718243498 au 0783243468

No comments: