Naibu waziri wa elimu philipo mulugo (kushoto)
Masoud Masasi , Chamwino
SHULE mbili za wilayani Chamwino ,mkoani Dodoma zimeiomba Serikali kuzipelekea vitabu vya kiada na ziada ili kukabiliana na matokeo mabaya ya mitihani.Shule hizo za Sekondari Mvumi Mission na ya Msingi ya wasioona Buigiri wilayani humo, zinakabiliwa na uhaba wa vitabu hivyo tofauti na shule nyingine .
Hayo yalibainishwa juzi na mmoja wa wanafunzi anayesoma kidato cha tatu katika shule ya Sekondari Mvumi, Fadhila Mvena aliposoma hotuba kwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo alipotembelea shuleni hapo.
Mvena alisema kuwa, wamekuwa wakipata taabu sana kutokana na kukosa vitabu pamoja karatasi za kusomea zinazotumia mashine ya nukta nundu na kusababisha wanafunzi hao kufanya vibaya katika mitihani yao.
Alisema awali wakiwa katika shule ya msingi wasioona ya buigiri tatizo hilo halikuwa kubwa sana kama lilivyo sasa, ambapo wanajikuta wakishindwa kufanya vizuri katika masomo yao kutokana na kukosa vitu muhimu kama hivyo.
“Shule yetu inakabiliwa na uhaba wa vitabu vya kiada na ziada mbali na hilo pia hatuna karatasi za kusomea zinazotumia mashine ya nukta nundu tunaiomba serikali itusaidie hili kwani inachangia kushuka kwa kiwango chetu cha elimu kutokana na uhaba huo kwa kuwa mitihani tunayofanya na wanafunzi wengine ni sawa , ila wenzetu wanavyo vitabu vya kutosha” alisema Mvena.
Aidha alisema wanafunzi wasioona nao wanahitaji kupata haki sawa na wengine ili waweze kuondokana na vitendo vya kukaa nyumbani na kuwa ombaomba mara baada ya kufeli mitihani yao.
Naibu Waziri alilikubali ombi hilo na kumwagiza Katibu wa Waziri kufikisha suala hilo kwa Waziri ili kutenga Sh1 milioni ya kununulia karatasi hizo ili ziweze kuwasaidia wanafunzi hao.

No comments:
Post a Comment