Tuesday, November 22, 2011

SERIKALI ITUPIE MACHO SHULE ZA CHEKECHEA ZA BINAFSI


Na mdau wa elimu
Kwanza napenda kumpongeza Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya ufundi kwa kazi nzuri anayoifanya kwa sasa kwa  kuzifunga shule zote zisizisajiliwa na si sizo na sifa za kuitwa shule.
Namuomba ndugu Waziri kwa mtindo na  kwa kasi  hiyo hiyo, azitupie macho shule za chekechea au awali  hapa nchini.
Iko siku  Tafa hili litakuja shuhudia  kupoteza idadi kubwa ya watoto hawa malaika ya Mungu, kufa ama kujeruhiwa kwa kuangukiwa na majengo haya yanayosomea watoto hawa.Nasema hivyo kwa sababu baadhi  ya  hizo  shule zinazoitwa shule za chekechea au shule za awali,  ni vituko tupu na kichefuchefu na  ni hatari.  Majengo yake ni mabanda ya uani ya nyumba za uswahilini au magofu hata sebule za nyumba za kuishi.Baadhi ya majengo hayo mapaa yake yamewekewa mawo ili yasiwezuke na upepo na yana vuja. Mvua zikinyesha ni balaa tupu.
Na  baadhi hayana hata madirisha ya kutosha kuingizia hewa.Hata sehemu au viwanja vya kuchezea watotohawa   hakuna. Baadhi ya shule hizi zinaendeshwa kienyeji mno.Mazingira yake hayafai kwa afya na ustawi wa mtoto.Watoto hawa wanalazimishwa kusoma hadi saa kumi kwa kutozwa hela za chakula cha mchana ambacho si  chakula bora.
Ugali maharagwe bila hata tunda.Isitoshe ikifika mchana watoto hawa  wanalazimishwa kulala chini au kwenye mkeka chakavu kwenye aridhi au sementi chakavu.Kuna hatari ya kuumwa mbavu na kupata maumivu ya viungo,kupata  mafua kwa vumbi.Baadhi ya vyoo ni  vibovu na ni hatari mtoto pia anaweza akatumbukia kwa vile vyoo vya mashimo.Hata baadhi ya walimu sidhani kama wana sifa za kufundisha  malaika hawa ali mrasdi mkono uende kinywani.
Waswahili wanasema  usipo ziba ufa utajenga ukuta. Serikali isipodhibiti hali hii mapema ,iko siku taifa  hili la wapole na  wanyonge litaingia katika majonzi ya kujitakia. Tusingoje  hadi mafa yatytokee ndipo tuanze kumtafuta mchawi.Yasije yakatokea  yale ya Tabora na Disko toto.

chanzo mwananchi

No comments: