Sunday, November 20, 2011

CHUO KIKUU CHA KIISLAMU CHAHITIMISHA MARA NNE



Baadhi ya wanachuo wa chuo kikuu cha kiislamu wakisubiri kupokea digrii zao

Chuo kikuu cha kiislamu (MUM) kilichopo mkoani morogoro jana kilifikisha mara ya nne katika mzunguko wa kuhitimisha wasomi ambapo wasomi mbalimbali walishuhudiwa wakipokea digrii zao majira ya saa tisa mpaka kumi jioni, wasomi hao ambao kwa namna moja ama nyingine walionekana wakiwa na furaha kwa kumaliza safari yao ndeefu sana ya kimasomo iliyokuwa na mikikimikiki mingi ambayo kwa uwezo wa mungu walifanikiwa kuivuka hivyo hawakuweza kuzuia furaha zao pale tu walipo maliza elimu yao hiyo jana.

Naye mmoja wa wahitimu hao ambae alipata fursa ya kuongea na mwandishi wa blog hii Bwana RASHIDI TEBE akiwa ameambatana na ndugu zake ambao wengi walitoka dar es salaam kwaajili ya kumsindikiza alisema kuwa anafurahi sana kwakuwa chuoni kuna mitihani mingi sana kwa mfano kuna mambo mengi ya kurudia mitihani (SUPLIMENTARY) ijulikanayo sana kama (SUP) kwa ufupi au kufutwa kabisa kwenye orodha ya wanaoendelea na masomo (DISCONTINUE) au maarufu kama (DISCO) vitu hivyo ni kawaida sana kwa chuoni ila wao wameweza kuepukana navyo hivyo wana kila sababu ya kufurahi.

Blog hii inawapongeza sana wahitimu hao na kuwataka wawe ni miongoni mwa walioelimika na sio wasomi pekee kwa kuepukana na kufanya kazi kifisadi na wawe ni wenye kufanya kazi kwa juhudi ili kuleta maendeleo si kwao tu bali na kwa taifa kwa ujumla 

No comments: