Friday, November 25, 2011

MBUNGE MURTAZA MANGUNGU ADANGANYA TAIFA

Mbunge wa Kilwa Kaskazini atuhumiwa kwa kudanganya taifa kuhusiana na sekta ya elimu: Umoja wa wanafunzi wa elimu ya juu waliotoka wilaya ya Kilwa,Mkoa wa Lindi,wameingia katika mvutano mkubwa na Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Murtaza Mangungu(CCM) wakimtuhumu kulidanganya taifa kuhusiana na suala zima la kusaidia sekta ya elimu. Umoja huo umesema kuwa mbunge huyo amekaririwa akisema kuwa amewapatia kiasi cha sh milioni 4.5 ili kusaidia kufundisha wanafunzi wa sekondari wilayani humo jambo ambalo walidai kuwa si kweli( Chanzo cha Habari: Tanzania Daima 22 Novemba 2011)

No comments: