Monday, October 31, 2011

WADAU WA ELIMU WALUMBANA VIKALI KWENYE SEMINA YA TGNP

                        Lilian Liundi (TGNP) mwenye laptop akiwa na wanasemina wakijadiliana kitu                                                           
KUSHUKA kwa ufaulu wa wanafunzi wa shule za sekondari kwa kidato cha nne, kuliibua mjadala mkali jijini Dar es Salaam baada ya makundi yaliyoshiriki semina iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia (TGNP) kutofautiana kuhusu sababu zake.  Hali hiyo ilijidhihirisha katika semina hiyo ya TGNP ambapo wachangiaji waliojitambulisha kuwa ni wanasiasa kutoka katika vyama vya CCM na Chadema waliposimama kuchangia.

Ofisa Mwandamizi wa CCM, Idara ya Mahusiano ya Kimatifa, Amos Robert ambaye alisimama na kuanza kutetea serikali ya CCM kwa kudai kuwa haisitahili kulaumiwa kwa kushuka kwa ufaulu huo.

 “Suala la kushuka kwa elimu serikali isilaumiwe pekee, Serikali ya CCM ni sikivu na inayo mazuri mengi imeyafanya katika awamu zote za uongozi wake”, alisema  Robert  na kuongeza “Wachangiaji wengi wanazungumzia shule za kata kuwa zina kiwango duni cha utoaji elimu,huo ni utekelezaji wa ilani ya CCM awamu ya kwanza ya kujenga shule, sasa mpango unaokuja ni wa uboreshaji shule hizo kwa kujenga maabara na kupeleka walimu”alisema.

Amos aliwataka wachangiaji kutambua kuwa hakuna mfumo wa elimu duniani usio na mapungufu na kusisitiza yeye ametumwa kutoka makao makuu ya chama ili kusikiliza mawazo ya wanaharakati na kuyafikisha makao makuu ili yakafanyiwe kazi.Kauli ya kada huyo wa CCM ilimuinua Mbunge wa SuzanLyimo9Viti Maalumu Chadema) ambaye kama mtangulizi wake alijitambulisha kuwa yeye ni mwanasiasa kutoka Chadema.

 Lyimo alisema kuhusu kushuka kwa elimu serikali ya CCM haiwezi kukwepa lawama sababu imevurugu mitalaa na kuwatelekeza walimu makusudi ili kuwafanya Watanzania wawe wajinga iweze kuwatawala. “Mimi ni mwalimu,walimu wamedharauliwa na kutelekezwa,mitalaa imevurugika,ziko wapi shule za sekondari za serikali ambazo ndizo zilizokuwa zikitamba kwa kutoa elimu bora,huu ni kuporomoka kwa elimu ni mpango wa Serikali ya CCM wenye lengo la kuwafanya watu wabaki  na maskini ili wao waendelee kutawala”alisema Lyimo.

 . Katika mjadala huo wachangiaji waliendelea kutofuatina juu ya nani wa kulaumiwa ambapo Hussen Bondei aliitetea serikali kuwa haistahili lawama katika hilo. Kwa upande wake alihoji sababu za wazazi kuruhusu uwepo wa shule za kata bila kuwa na mabweni na kusema hali hiyo inatoa fursa kwa watoto hao kupata mimba wakiwa mashuleni.

“Serikali imekosea! mimi sitaki kusema hivyo, je wazazi wana moyo wa kuchangia  katika elimu?”alihoji Bondei.
Naye Lecat Nkya aliyejitambulisha kuwa ni Mwalimu aliwatupia lawamu wananchi kwa kuwachagua viongozi wasiotimiza wajibu wao kwa kushindwa kutambua umuhimu wa elimu hapa nchini.

No comments: