Monday, October 31, 2011

RAIS WA CWT ATOA TAMKO KWA SERIKALI JUU YA WALIMU WANAOIDAI SERIKALI



                   Kulia ni Mh. Rais Jakaya Kikwete katikati ni ndg Gratian Mkoba na mwisho na aliyekuwa
                                          waziri wa elimu Prof.   Jumanne Magembe (RUVUMA)

Serikali imepewa muda wiki moja tu (mpaka tarehe 5/12/2011)kutoka leo wawe tayari wameshafikia sehemu muhimu juu ya kuwalipa walimu wote ambao wanaendelea kumegwa na jinamizi la kuadai serikali kwa miaka mingi sasa, hayo yamesemwa na Rais wa chama cha walimu ndugu Gratian Mukoba alipokuwa akijibu swali juu ya namna wanavyoendelea kufuatilia madeni hayo ya walimu kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini mwanza hivi karibuni,
 Aidha amesema kuwa mpaka itakapofika tarehe 15/12/2011 kama bado hakuna maelezo ya kueleweka basi ataitisha baraza lake kuona namna watakavyoamua kufanya juu ya ukimya huo wa serikali na maamuzi wanayoyachukua bila kushirikiana na chama hicho, akisisitiza zaidi amesema kuwa serikali imesitisha uhakiki kinyume na makubaliano ya kwamba uhakiki inabidi uishe mwezi wa 11 hivyo basi kwa mwalimu yoyote ambae anaidai serikali apeleke madai hayo kwenye ofisi za chama  cha walimu na wao kama viongozi watayapeleka madeni yote ambayo walimu wanadai kwa serikali na kusema kuwa serikali ni lazima ilipe madeni hayo.
Hii ni kauli ya pili ya bwana Gratian Mukoba kuishinikiza serikali kwa muda wa miezi mitano kwani awali july mosi Mukoba aliipa serikali muda wa mwezi mmoja kuhakikisha inawalipa walimu kiasi cha shilingi 13 bilioni vinginevyo itaitisha mgomo nchi nzima.

No comments: