Na mdau wa elimu
SERIKALI inatarajia kuajiri walimu wapya 23,027 wa ngazi ya Cheti, Stashahada na Shahada katika Halmashauri mbalimbali hapa nchini kuanzia mwenzi huu.Walimu hao wa shule za msingi, yaani ngazi ya Cheti ni 10,595, Stashahada ni 5,848 na Shahada ni 6,584 ambao jumla yao ni 23,027 ambao walikuwa hawajaariwa, hivyo kuilalamikia serikali kwa kutowajulisha hatima ya ajira zao.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo alisema kuwa Wizara yake imeishakamilisha uchambuzi wa majina na kuyapeleka Utumishi kuomba kibali ambapo Tamisemi ndio itakayopanga vituo vya kazi kwa walimu hao.
“Kwa upande wa Wizara yangu tumeishakamilisha utaratibu wote na sasa ni Utumishi na Tamisemi, lakini ninavyojua ajira hizo zitatangazwa muda wowote kuanzia sasa maana haiwezi kufika Desemba bila walimu hao kuripoti katika vituo vyao vya kazi,” alisema Mulugo.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia elimu katika Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Jumanne Sagini alisema kuwa taratibu za ajira tayari zimekamilika na kwamba wamepokea majina ya walimu 23,027 na kwamba ifikapo Novemba 15 mwaka huu ajira za walimu hao zitakuwa zimetangazwa.
“Ni kweli tumepokea majina ya walimu ambao wanazo sifa na vigezo vya ualimu jumla yao ni 23,027 wa shule za msingi na Sekondari kwa hiyo kuanzia sasa walimu hao watatangaziwa vituo vyao vya kazi ambavyo watatakiwa kuripoti,” alisema Sagini.
Alisema kuwa sababu ya walimu kuchelewa kupata ajira ni pamoja na uhakiki wa vyeti na kuepuka kuwapangia kazi bila kuwa na fedha za kuwalipa mara wanaporipoti kazini na kwamba kwa sasa hakuna mwalimu atakayekwenda kazini bila kupata malipo yake.
Alisema kuwa siku za nyuma serikali imekuwa ikionekana kuwa na uhasama na walimu baada ya wengi kufika kazini na kukuta hakuna maandalizi yoyote na mishahara yao imekuwa ikichelewa sana, hali ambayo imekuwa ikisababisha walimu wengine kutoroka kazini.
“Mwaka huu hatutaki uhasama na mwalimu yeyote kama ilivyotokea miaka ya nyuma ndio maana wamechelewa kupangiwa vituo vya kazi ili serikali ijiandae vizuri ili kila mwalimu atakapokwenda kazini apate haki zake za msingi ili kuondoa malalamiko yaliyokuwa yakijitokeza,” alisema Sagini.
Alisema kuwa hadi Novemba 15 mwaka huu majina ya walimu wote yatakuwa yamewekwa kwenye tovuti ya Tamisemi ili kila mwalimu ajue Halmashauri aliyopangiwa na kuwataka walimu wawe na subira wakati utaratibu huo ukiendelea kufanyika.

No comments:
Post a Comment